Pages

Wednesday, October 30, 2013

BLATTER AMUOMBA RADHI RONALDO BAADA YA KUSEMA ANAMPENDA MESSI

ronaldo 0fbcd
RAIS wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Sepp Blatter ameomba radhi kwa Cristiano Ronaldo baada ya mshambuliaji huyo wa Real Madrid kumchamba katika ukurasa wake wa Facebook.

Mapema Blatter alitoa hotuba iliyomkera Ronaldo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Oxford, Uingereza. Katika majadiliano yake na wanafunzi hao, Blatter alielezea mapenzi yake kwa Lionel Messi, na akaweka kando kiti chake cha Urais FIFA na kumshambulia kibinafsi Ronaldo. Blatter pia amesemekana kumpiga dongo nyota huyo wa Madrid kwamba anatumia fedha zake nyingi kupamba nywele zake.
Hiyo imemfanya Mreno huyo, aliyeingizwa kwenye kinyang'anyiro cha tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia 2013, Ballon d'Or, aposti katika ukurasa wake wa Facebook: "Video hii inaonyesha dhahiri heshima na namna ambavyo FIFA wapo kwangu, kwa klabu yangu na nchi yangu,".
"Wote ni wachezaji wa kipekee, lakini wako tofauti kabisa. Ni nyota tofauti kabisa.
"Lionel Messi ni kijana mzuri, ambaye kila baba na kila mama angependa kumpeleka nyumbani. Ni mtu mzuri, ana kasi sana, na anacheza vizuri. Ni mtu wa aina hiyo, kijana mzuri. Kitu ambacho kinamfanya awe maarufu, na kiasili wakati wote ataendelea kupata kura nyingi kwa sababu anacheza vizuri na kufunga mabao.
"Mwingine mmoja naye (Ronaldo) ni kitu fulani pia. Ni kama kamanda anavyocheza uwanjani. (Blatter akawa anaonyesha mifano ya uchezaji wake na kushangiliwa).
"Huu ni upande mwingine wa soka na vizuri kuwa na makamanda uwanjani. Hawashibihiani na hicho ndicho kinaubeba mchezo wa soka. Mmoja anatumia fedha nyingi kutengeneza nwele zaidi ya mwingine, lakini hiyo haijalishi.
"Siwezi kusema nani ni bora- kutakuwa na shindano mwaka huu tena Ballon d'Or. Nawapenda wote, lakini nampenda Messi,".
"Mambo hadharani sasa. Namtakia Bwana. Blatter afya na maisha marefu, aendelee kuona na kushuhudia mafanikio ya timu na wachezaji anaowapenda,".
Baadaye Blatter akaandika kwenye Twitter: "Dear @Cristiano. Naomba radhi kwako kama ulichukizwa na jibu la swali wangu katika tukio binafsi Ijumaa. Sikuwa na maana ya kukuumiza wewe.
"Nina heshima Real Madrid @cristiano na tuna vipaji vingi katika mchezo huu duniani, ukiwemo wewe. Kila heri,".
Hatua hii inakuja baada ya Real Madrid kuiandikia FIFA ikimtaka Blatter aome radhi kwa maneno yake juu ya Ronaldo.
Katika mkutano na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Sevilla, kocha wa Madrid, Carlo Ancelotti amesema: "Rais [Florentino Perez] ametuma barua FIFA kumtaka Blatter kuomba radhi kwake kauli zake juu ya Cristiano.' Chanzo: binzubeiry

No comments:

Post a Comment