Mwenyekiti
wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard kulia
akitoa msimamo wa wanahabari dhidi ya gazeti la Rai na mbunge Msigwa leo
,kushoto ni katibu mtendaji wa IPC Francis Godwin
Wanahabari
Clement Sanga kushoto akiwa na mwakilishi wa New habari {2006} Ltd
wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania , Rai na Bingwa mkoa wa Iringa
Mercy Mwalusamba wakati wa kikao cha cha wanahabari mkoa wa Iringa jana
kujadili habari zilizoandikwa na gazeti la rai jumapili
Wanahabari wakifuatilia kwa makini kikao hicho
WANAHABARI
mkoani Iringa wamekanusha vikali habari zilizoandika na gazeti la Rai
toleo namba 1067 la jumapili wiki iliyopita kuwa wanahabari mjini Iringa
wamehongwa fedha na viongozi wa CCM mkoa wa Iringa ili wasiandike
habari ya msaidizi wa mbunge Wiliam Lukuvi Bw Thom Malenga kukamatwa kwa
tuhuma za kujihusisha na ujangili.
Wahanabari hao katika kikao chao
kilichofanyika leo katika ofisi za klabu ya waandishi wa habari mkoa wa
Iringa (IPC) mbali ya kukanusha habari hizo kuwa zimeandikwa kwa lengo
la kuchafua tasnia ya habari mkoa wa Iringa ila bado wanalitaka gazeti
la Rai na mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa
kuwataja waandishi waliohongwa na viongozi wa CCM mkoa wa Iringa kabla
ya wanahabari hao hawajachukua hatua zaidi dhidi ya gazeti la rai pamoja
na mbunge Msigwa."Kilichoandikwa na gazeti la Rai jumapili kuhusu wanahabari Iringa hawajatutendea haki na wametuvunjia heshima yetu kwa wadau wa habari mkoa wa Iringa na nje ya mkoa wa Iringa.....ila tunachotaka Rai kuwataja waandishi hao waliohongwa ili sisi kwa sisi kama wanahabari kuanza kuchukuliana hatua ....wakishindwa kufanya hivyo ndani ya siku 14 kuanzia leo jumanne tutawafikisha baraza la habari Tanzania (MCT)"
Walisema wanahabari hao katika tamko lao la pamoja lililotolewa na mwenyekiti wa IPC Frank Leonard kuwa taarifa hiyo imechafua vibaya wanahabari Iringa na sio wacache ni wote kutokana na jinsi ambavyo gazeti hilo lilivyoandika habari hiyo tena mbaya zaidi mwandishi wa habari hiyo hakuweza kuwatendea haki wanahabari Iringa hata kwa kuonyesha kuwahoji katika habari yake hiyo.
Leonard alisema kuwa si kweli kama wanahabari Iringa walishindwa kuandika habari hiyo ya kukamatwa kwa Malenga isipo kuwa wanahabari Iringa ni makini na hawakutaka kuandika habari kwa kukurupuka hivyo walitaka kabla ya kuandika kuweza kumpata msemaji wa kikosi hicho cha kupambana na ujangili ili kulizungumzia hilo kabla ya kuandika jambo ambalo wao kama wanahabari walikuwa wakilisikia mitaani bila kuwa na uhakika.
Uandishi wa habari mzuri ni pamoja na kuzingatia maadili ya uandishi na sio kuandika bila ya kuwa na uhakika wa kile unachokiandika .
Hata hivyo alisema kwa kuwa mbunge Msigwa amenukuliwa katika gazeti hilo kama ndio msemaji wa jambo hilo wao kama wanahabari watamwandikia barua mbunge huyo ili kusaidia kuwataja wanahabari waliohongwa pesa vinginevyo wao kama wanahabari wa mkoa wa Iringa hawatamvumilia mbunge Msigwa katika hilo .
Pia alisema kuwa suala hilo kwa sasa ameachiwa mwanasheria wa IPC ili kulifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuwaandikia barua Rai na mbunge Msigwa kuwataka kuthibitisha ukweli wa kilichoandikwa dhidi ya wanahabari mkoa wa Iringa.
No comments:
Post a Comment