Haya ni maji machafu yaliyogeuka na kuwa mto baada ya wananchi kutoa taarifa kwa DAWASCO bila kupta msaada wowote
Inasikitisha maana eneo hili lililoko nyuma ya maghorofa ya JWTZ maeneo ya Mwenge sasa maji machafu yamekuwa kama mto
Huu
ndio uchafu unaotoka kwenye chemba hizo ila cha kusikitisha wananchi
wametoa taarifa zaidi ya mara tano huko DAWASCO bila mafanikio yoyote
Watoto sasa wameugeuza na kuwa mto wa kuloa samaki
Hii ni mojawapo ya chemba inayotoa maji mchafu
Inasikitisha sana DAWASCO kutokuja kuzibua chemba za maji taka na kupelekea wananchi wanaoishi eneo hilo kuwa kero
Tazama kinyesi kikiwa kimejitenga kwenye maji hayo machafu
Vingozi wa DAWASCO mmeliona hili?
Mbaya zaidi simu imepigwa kwa muhusika moja kwa moja mida ya saa kumi lakini nae hakupokea simu hiyo kwa kuona kuwa ni kero kwake maana wananchi wataomba swala hilo hilo
sasa je hili ni jukumu la nani? wananchi wamlilie nani? je kama hawa wahusika wangekuwa wanakaaa mtaa huu ambao unaitwa ni mtaa wa mavi wangependaaa
"Hebu tusaidieni jamani tunakufa na hii harufu mbaya, hatulali na tunaogopa magonjwa ya mlipuko." alisema mmoja wa wakazi wa eneo hili
na dar yetu
No comments:
Post a Comment