DEREVA tax mkazi wa Chalinze
Mohamed Mrisho (27) ameuawa kikatili kwa kukatwa shingo na kutenganishwa na
kiwiliwili cha mwili huko kijiji cha Bago kata ya Kiwangwa wilayani Bagamoyo
Watuhumiwa wa tukio
hilo wametajwa kuwa ni watu wawili wa kiume ambao walifika majira ya saa 1.15
usiku kituoni Chalinze kisha kumtaka dereva huyo awasafirishe kwenda kata
ya Kiwangwa wilayani humo.
Kamanda wa Polisi
mkoani Pwani Ulrich Matei amethibitisha tukio hilo ambapo amesema
limetokea majira ya saa moja usiku wa kuamkia jana wakati dereva huyo akiwa
katika shughuli zake za kusubiri wateja wa huduma hiyo ya tax.
Matei amesema tayari
mtuhumiwa mmoja aliyemtaja Peter Charles (21) anashikiliwa na jeshi hilo huku
mwenzake aliyetajwa jina moja la John akiendelea kusakwa.
Matei amesema ametaja
gari walilolikodi watuhumiwa hao ni T 426 BUT aina ya Avenlit na lilikuwa
linaendeshwa na marehemu huyo.
Aliongeza kuwa abiria
hao walitembea na hilo gari lakini hawakufika nalo mbali kwani walipata ajali
na kutumbukia mtaroni huko Msata.
Kamanda huyo amesema
kama ilivyo ada ikitokea ajali watu hujitokeza kusaidia na ndivyo ilivyokuwa
kwa watuhumiwa hao wananchi walifika kutoa msaada lakini walipokaribia karibu
mmoja wa watuhumiwa aliyetajwa jina moja la John alikimbia na hivyo walimkamata
Peter na walipomuhoji walibaini si mali yao hivyo kutoa taarifa Polisi.
Amesema askari
walifika eneo la ajali na kufanya upekuzi ambapo walikuta kisu yenye damu ndani
ya gari na kumuhoji mtuhumiwa ambapo aliwapeleka askari hao eneo walikofanyia
mauji na kukutwa mwili wa marehemu pembeni mwa barabara na pembeni mwake
kulikutwa pia kisu kingine kilichotapakaa damu.
Mwili wa
marehemu ulifanyiwa uchunguzi wa daktari kisha kukabithiwa ndugu kwa mazishi.
No comments:
Post a Comment