Pages

Thursday, October 3, 2013

DIAMOND ​AKABIDHI IPAD KWA MSHINDI MKALI WA KUCHEZA NGOLOLO STYLE


001 RBT ac801
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul "Diamond Platinumz"akimkabidhi Ipad yenye thamani ya shilingi Milioni Tsh 1.2 mshindi wa dansi ya Ngololo Bw.Faudhu Kiobya kupitia ukurasa wa kijamii wa instragram wa Vodacom Tanzania,mara baada ya kumalizika droo ya tatu ya shindano la miito ya simu.Washindi 35 kila mmoja amejishindia Sh 50,000.Anaeshuhudia katikati ni Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Bw.Mathew Kampambe, Chanzo Matina Nkurlu 
003 RBT 3bd6d
Mshindi wa dansi ya Ngololo Bw.Faudhu Kiobya,aliejishindia Ipad kwa kutuma video katika ukurasa wa kijamii wa instragram wa Vodacom Tanzania,akionesha Ipad yake kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)aliejishindia na kukabidhiwa rasmi na Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul "Diamond Platinum"(kulia)wakati wa droo ya tatu ya shindano la miito ya simu,ambapo washindi 35 kila mmoja wamejishindia Sh 50,000.katikati ni Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Bw.Mathew Kampambe.
004 RBT 0dd1b
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul "Diamond Platinum"(kushoto)pamoja na Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Bw.Mathew Kampambe,(kulia)wakionyeshwa kurasa mbalimbali za Ipad na mshindi wa dansi ya Ngololo Bw.Faudhu Kiobya,aliejishindia mara baada ya kutuma video yake katika ukurasa wa kijamii wa instragram wa Vodacom Tanzania,na kukabidhiwa rasmi na msanii huyo baada ya kumalizika kwa droo ya tatu ya shindano la miito ya simu.Jumla ya washindi 35 kila mmoja wamejishindia Sh 50,000.

No comments:

Post a Comment