Pages

Tuesday, October 1, 2013

DVD ZA SHAMBULIO A WESTGATE MALL ZINAUZWA....KWELI DUNIANI KUFA KUFAANA....KAMATA FURSA


Tovuti ya NairobiWire imeripoti kuwa  baadhi ya wafanyabiashara na wachuuzi katika eneo la mji mkuu wa Nairobi, River Road na barabara nyinginezo, wameanza kuuza nakala za DVD za shambulio la kigaidi la Jumamosi ya tarehe 21, Septemba 2013, lililosababisha maafa makubwa nchini Kenya na kuleta simanzi katika maeneo mbalimbali duniani.


Inawezekana kabisa ikawa ni nafasi ya kujipatia kumbukumbu lakini inashangaza kidogo uharaka wa ufyatuaji santuri hizo kabla ya taarifa kamili kuhusu tukio hilo haijatolewa rasmi kwani  inasemekana DVDs zinazouzwa sasa katika majina tofauti (kama unavyoona kwenye picha) ni mkusanyiko wa taarifa mbalimbali zilizoripitiwa hadi saa kuhusu tukio hilo. Kwa mapungufu hayo, pengine ndiyo zitatoka parts 1, 2, 3, 4 mpaka infinity.


Najaribu kulinganisha miaka kama kumi hivi na kurudi nyuma iliyopita, hadi kwenye tukio la mwaka 1998 la kulipuliwa kwa balozi mbili za Marekani nchini Kenya na Tanzania, najiuliza kama wakati ule watu walikuwa wazubaifu wa 'kuchangamkia' fursa ya ujasiriamali katika maafa na msiba na vilio vya wengine au waliwakosesha watu kumbukumbu muhimu.

Pengine ndiyo mabadiliko ya nyakati hizi, kila jambo kama wasemavyo wenyewe, 'inategemea mtazamo wako.'

No comments:

Post a Comment