Pages

Tuesday, October 1, 2013

TAARIFA KUHUSU KIFO CHA MARK2 B,HISTORIA YAKE KWA UFUPI NA TARATIBU ZA MAZISHI LEO


Msanii aliyekuwa akiunda kundi la Wateule Simba aka Mark 2 B amefariki dunia leo huko kwao Yombo baada ya kuugua ugonjwa wa miguu kujaa maji,hii ni kwa mujibu wa kaka yake anayejulikana kama Msafiri.Simba ambaye jina lake halisi ni Malick Ahmed alizaliwa Jan 20 mwaka 1980 akiwa mtoto wa mwisho katika familia yao.Wimbo wa 'Ndani ya Party' wa Solo alioshirikishwa Simba ni kati ya ngoma ambazo alizoshirikishwa zilizofanya vizuri.Simba ambaye pia alikuwa ni produza mwaka jana alichaguliwa kuwania tuzo za Kilimanjaro kupitia wimbo wake wa 'Paradise'.

Kaka wa marehemu amesema kuwa marehemu anatarajiwa kuzikwa kesho saa 4 asubuhi huko Yombo.Kaka huyo alisema kuwa mtu akipanda magari ya Yombo ashuke kituo cha Abiola na aulizie kwa Mzee Moha au kwa kina Malick.Mara ya mwisho marehemu pia alikuwa akifanya kazi katika studio za Baucha Rec.Mmiliki wa Baucha Rec,produza Baucha alinambia kuwa marehemu aliondoka katika studio yake kuanzia mwezi wa 4 mwaka huu kutokana na kuanza kuumwa.Kwa msaada wa ANNA PETER

Marehemu alisoma shule ya msingi Kurasini,baadae Sekondari Al Haramaini mpaka mwaka 1997 ambapo alipomaliza ndo alianza kujiingiza kwenye muziki kwa kushiriki katika matamasha mbalimbali ya muziki.
 
#RIP SIMBA TUKO NYUMA YAKO

No comments:

Post a Comment