Silaha zilizokamatwa.
OPERESHENI
Maalumu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu kukabiliana na vitendo vya
Ujambazi, Ujangiri wa uwindaji haramu pamoja na wahamiaji haramu umefanikisha
kukamatwa kwa silaha 45, zikiwemo za Kivita na 17 za kienyeji na risasi
892 na magazine 24 huku watuhumiwa sugu wa ujambazi na ujangiri
wakitiwa mbaroni.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu Salum Msangi.
Silaha zilizokamatwa za kisasa na za kienyeji.
Shehena ya risasi zilizo kamatwa.
Silaha zilizotengenezwa kienyeji.
Akizungumza
jana mbele ya waandishi wa Habari ofisini kwake, Kamanda wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Simiyu Salum Msangi alisema kuwa opresheni hiyo ilitokana
na kuwepo vitendo vya uhalifu katika Wilaya tano za Mkoa huo na kwenye
maeneo ya mbalimbai ya Mapori Tengefu ya Uwindaji kwa kipindi cha mwaka
moja tangu kuanzishwa kwake Desemba 2012.
Kamanda
Msangi alieleza kuwa miongoni mwa silaha hizo 45 na magazine 28
zilikamatwa ni pamoja na SMG 7 risasi 763 na G3 moja ikiwa na risasi
zake 35 iliyokuwa ikitumiwa na mwanamke mmoja aliyekamatwa Hollo Mabuga
(28) mkazi wa Wilayani Bariadi, silaha nyingine 13 zilisalimishwa kwa
hihali na baadhi ya watu waliokuwa wakizimiliki kinyume na
sharia,Short-Gun saba, Gobole 17 na SAR moja.
“Tumeweza
pia kumkamata mtuhumiwa hatari wa matukio ya uhalifu ambaye hivi
karibuni aliachiwa kutoka Gerezani lakini tukapata taarifa za raia wema
kuwa amekuwa akijihusisha na ujangiri na ujambazi ambaye ni Masanja
Sumuni, tukaweka mtego na kufanikiwa kumkamata akiwa na SMG moja na
risasi 96 huku mke wake Hollo Mabuga akikutwa pia na silaha” alisema.
Kufuatia
operesheni hiyo Jeshi hilo pia limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu
wanne katika maeneo ya Wilaya ya meatu huku zaidi ya watu kumi
waliokuwa wakijihusisha na ujangiri wakikutwa na nyara za serikali ikiwa
niza wanyama waliopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Mapori ya
Akiba katika Wilaya za Meatu, Maswa na Itilima.
“Tumeunda
kikosi kazi ambacho pia kinaendelea na operesheni ya kuwakamata
wafugaji na mifugo yao ambao wamekuwa wakichungia mifugo ndani ya eneo
la Hifadhi ya Serengeti ambapo zaidi ya ng’ombe wengi walikamatwa na
kutozwa faini ambapo zaidi ya shilingi milioni 180 zilipatikana huku
watu wanaoendesha vitendo vya ujangiri wakiuwa tembo na wamyama na kuuza
kwa wananchi wa maeneo ya jirani” alisema Kamanda.
Kamanda
Msangi amewataka wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kutoa taarifa
za siri zitakazowawezesha kuwakamata wahalifu na wahamiaji haramu
katika maeneo yote ya Wilaya za Meatu, Maswa, Bariadi, Itilima na Busega
huku makakati wa kuanzisha vikosi kazi kila tarafa ukiwa mbioni
kukamilika ili kuimalisha ulinzi kwa wananchi na mali zao.CHANZO TANZANIANEWS
No comments:
Post a Comment