Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) Unasikitika
kuwaarifu Wakazi wa Jiji na Wananchi kwa ujumla kusitishwa huduma
treni ya Jiji ( Dar- Ubungo Maziwa) kwa siku ya leo ya Alhamis Oktoba
03, 2013. Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia ajali ya kichwa cha treni
hiyo kugongwa na lori jana Oktoba 2, 2013 saa 12:30 jioni katika
makutano ya reli Buguruni.
Ajali
hiyo imesababisha kuharibika kichwa cha treni na kuhitaji matengenezo
kabla ya kuendelea na huduma. Uongozi wa TRL unaahidi kusimamia
matengenezo kwa wakati ili huduma za treni za Jiji zirejee mapema kesho
Ijumaa Oktoba 04, 2013. Kufuatia ajali hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa
zaidi ya lori kupinduka na kuharibika kichwa cha treni.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ,
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji
Mhandisi Kipallo Amani Kisamfu,
Dar es Salaam
Oktoba 03, 2013.
No comments:
Post a Comment