Kikao cha baraza la madiwani la hamshauri ya wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza leo kimetawaliwa na vurugu na mabishano hali iliyopelekea kuvunjika kwa kikao hicho.
Vurugu na kurushiana maneno makali, zilianza baada ya meya wa halmashauri ya wilaya hiyo, Henry Matata kutoka chama cha Demokrasia na maendeleo alipotoa amri ya kuwafukuza kwenye kikao madiwani wawili kutoka chama cha Demokrasi na maendeleo (chadema).
Meya huyo ambaye mefungua kesi mahakamani ya kupinga kuvuliwa uanachama wa chadema, aliwataka madiwani hao kutoka nje kwa kile alichoeleza kuwa alikwisha wavua wadhifa wa udiwani kwa kitendo chao cha kugomea kuhudhuria vikao vya baraza bila kuiomba ruhusa kwa meya huyo
Vurugu hizo zilipelekea kushindwa kufanyika kwa kikao hicho ambapo madiwani hao wameeleza masikitiko yao kwa serikali kushindwa kuchukua hatua dhidi ya Meya huyo.CHANZO JAMII FORUM
CG MWENDA APITA MLANGO KWA MLANGO KUZUNGUMZA NA WALIPAKODI IGUNGA
-
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda
akiwa ziarani wilayani Igunga mkoani Tabora February 06 mwaka huu amepita
mlang...
7 hours ago
No comments:
Post a Comment