STRAIKA wa Yanga, Reliants Lusajo ndiye mchezaji msomi kuliko wote ndani ya kikosi hicho lakini amekiri kwamba ana changamoto kubwa ya kupata namba ya kudumu.
Lusajo amemaliza masomo yake ya Shahada (digrii)
katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi kilichopo mkoani Kilimanjaro
alikokuwa akisoma Shahada ya Ugavi (Bachelor of Arts in Procurement).
Mchezaji huyo amekosa michezo 10 ya ligi msimu huu
kwa kuwa alikuwa akimalizia ripoti yake ya Utafiti (Research) kama
sehemu ya masomo yake na mwezi ujao atatunukiwa shahada yake ya kwanza
kwenye mahafali ya chuo hicho.
Lusajo anakuwa mchezaji raia wa Tanzania, mwenye
elimu zaidi ya wachezaji wote wanaocheza Ligi Kuu kwa sasa ingawa
anazidiwa kidogo na kipa wa Toto Africa, Erick Ngwegwe ambayo iko Ligi
Daraja la Kwanza.
Uchunguzi wa Mwanaspoti umebaini kwamba wachezaji
wengi wa klabu za Ligi Kuu wameishia darasa la saba, kidato cha pili,
kidato cha nne na wachache wana elimu ya cheti.
“Nlifurahi kucheza kwa mara ya kwanza Ligi Kuu
baina ya Yanga na Mgambo JKT, ligi ni ngumu na inahitaji mtu kufanya
kazi kwa juhudi kubwa. “Yanga ina wachezaji wazuri na wenye uzoefu
mzuri, nafikiri kwa kwa sasa nimemaliza masomo yangu hivyo nitahakikisha
nafanya kazi yangu ya mpira kwa kujituma,” alisema Lusajo.CHANZO MWANASPOTI
No comments:
Post a Comment