Mwenyekiti
Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika
Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na
Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana
(katikati) akizungumza na wajumbe wa RECSA (hawapo pichani) katika
mkutano wao unaofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ambaye
leo anatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti RECSA ambapo anatarajiwa kuiongoza
kwa kipindi cha miaka miwili. Kulia ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo,
Theoneste Mutsindashyaka. Mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo.
Wajumbe
wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika
Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA)
wakiwa katika chumba cha mkutano wakijadili masuala mbalimbali ya jinsi
ya Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu katika
nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea,
Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania. Mkutano huo unafanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam ambapo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (meza kuu-kushoto)
anatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti wa RECSA kutoka kwa Mwenyekiti
anayemaliza muda wake leo, Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda,
Sheikh Mussa Fazil Harerimana (meza kuu-katikati).
Wajumbe
wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika
Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA)
wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano wa unaofanyika
katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam kufunguliwa. Wapili
kushoto waliokaa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel
Nchimbi ambaye leo anatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti wa RECSA kutoka kwa
Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini
Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana (wakatikati). Picha na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment