Athumani Nyamlani
Jamal Malinzi
Na Daniel Mbega
LEO hii ulimwengu wa soka unasikilizia matokeo ya uchaguzi mkuu wa Shirikisho la
Kandanda Tanzania (TFF)unaofanyika kwenye ukumbi wa NSSF Waterfront jijini Dar es Salaam.
Kufanyika
kwa uchaguzi huu ni mafanikio mengine ya kuondoa sintofahamu
iliyokuwepo baada ya kuahirishwa mara kadhaa kutokana na sababu
mbalimbali, zikiwemo za wagombea kukata rufaa FIFA kupinga kuenguliwa.
Lakini sasa mambo yote yako sawa na jana TFF ilifanya Mkutano wake Mkuu kabla ya kuelekea uchaguzi huu wa leo.
Rais
anayemaliza muda wake, Leodegar Chillah Tenga, ameendelea kuiweka rekodi
yake safi katika soka la Tanzania tangu alipokuwa anacheza soka na hata
kuiongoza Taifa Stars kwenye Kombe la Mataifa Afrika kule Lagos,
Nigeria mwaka 1980.
Tumeona
mafanikio mengi katika miaka nane aliyokuwepo madarakani, ingawa wapo
watu ambao wanaendelea kubeza. Duniani hakuna anayeweza kuridhika kwa
asilimia 100, hivyo ni mambo ya kawaida kabisa haya.
Soka
lililokosa mwelekeo wakati wa iliyokuwa FAT lilibadilika ghafla tangu
mwaka 2004 TFF ilipoundwa na uongozi mpya kushika madaraka.
Kitu
pekee ambacho kimeonekana kuwa dhahiri ni kwamba, uongozi wa soka sasa
unashikiliwa na wanaoujua mchezo wenyewe, tofauti na miaka ile ambapo
yeyote mwenye ushawishi – wa fedha na maneno – aliweza kuongoza hata
kama haweza kupiga danadana mpira.
Wagombe
wa nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa leo ni Athuman Jumanne Nyamlani
na Jamal Emily Malinzi (Rais), Imani Omari Madega, Ramadhan Omar Nassib
na Wallace Karia (Makamu wa Rais).
Kwa
upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Kalilo Samson (Kanda namba 1-
Geita na Kagera), Jumbe Odessa Magati, Mugisha Galibona, Samwel Nyalla
na Vedastus Lufano (Kanda namba 2- Mara na Mwanza), Epaphra Swai na
Mbasha Matutu (Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu).
Ali
Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omar Walii Ali (Kanda namba 4- Arusha na
Manyara), Ahmed Idd Mgoyi na Yusuf Hamis Kitumbo (Kanda namba 5- Kigoma
na Tabora), Ayubu Nyaulingo na Blassy Mghube Kiondo (Kanda namba 6-
Katavi na Rukwa), Ayoub Shaibu Nyenzi, David Samson Lugenge, John
Exavery Kiteve, Lusekelo Elias Mwanjala (Kanda namba 7- Iringa na
Mbeya).
James
Patrick Mhagama na Stanley William Lugenge (Kanda namba 8- Njombe na
Ruvuma), Athuman Kingombe Kambi, Francis Kumba Ndulane na Zafarani Mzee
Damoder (Kanda namba 9- Lindi na Mtwara), Hussein Zuberi Mwamba, Stewart
Ernest Masima, Charles Komba (Kanda namba 10- Dodoma na Singida), Farid
Nahdi, Geofrey Irick Nyange, Juma Abbas Pinto, Riziki Juma Majala) na
Twahil Twaha Njoki (Kanda namba 11- Morogoro na Pwani).
Davis
Elisa Mosha, Khalid Abdallah Mohamed (Kanda namba 12- Kilimanjaro na
Pwani), Alex Crispine Kamuzelya, Kidao Wilfred Mzigama, Muhsin Said
Balhabou na Omary Isack Abdulkadir (Kanda namba 13- Dar es Salaam).
No comments:
Post a Comment