Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia ni
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ameamua
kukakatiza ziara yake nchini Denmark ili kushiriki msiba wa dada yake
mpendwa aitwaye Grace Mbowe aliyefariki dunia juzi (Jumapili). Marehemu
Grace alifariki kwa ajali ya gari katika kata ya Kabuku wilayani
Handeni, mkoani Tanga. Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi.
Amen!
No comments:
Post a Comment