Ndung'u Gethenji mwenyekiti wa kamati ya Bunge inayochunguza
shambulio hilo pia amesema mwili mwingine ambao umepatikana unawezekana
kwa kiasi kikubwa ukawa ni wa mmoja wa wanajeshi.
Mamlaka ya Kenya kwa sasa inaendelea na uchunguzi wa kisayansi wa miili hiyo.
Karibu watu wapatao 67 walifariki dunia wakati magaidi wanaodhaniwa
kuwa ni wa kundi la wanamgambo wa Al Shaabab waliposhambulia kituo
hicho Septemba 21 mwaka huu.
Shambulio hilo lilisababisha eneo hilo kuzingirwa kwa siku nne ambapo pia sehemu kubwa ya kituo hicho cha biashara iliharibiwa.
Mamlaka ya Kenya imeyataja majina manne ya watuhumiwa wa shambulio hilo, japo hawajatoa ufafanuzi zaidi.
Bado haijajulikana kama magaidi waliofanya shambilizi hilo kama
walitoroka au la na pia imekuwa ni vigumu kujua idadi ya magaidi
waliohusika kwenye tukio hilo.
No comments:
Post a Comment