Mwili
wa marehemu Anthery Mushi aliyejiua kwa kujipiga risasi mwishoni mwa
wiki iliyopita, umekutwa na risasi mbili, moja ikiwa kwenye ubongo na
nyingine kwenye jeraha lililo pembeni ya sikio.
Risasi
hizo zimebainika kufuatia uchunguzi uliofanywa na madaktari wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na maofisa wa Jeshi
la Polisi.
Isaya Mushi, msemaji wa familia ya Mushi alisema mwili wa ndugu yao ulikutwa na risasi hizo baada ya uchunguzi uliofanywa juzi.
Alisema hayo wakati wa kuuaga mwili wa Mushi tayari kuusafirisha kwenda Kijiji cha Ongoma, Uru, mkoani Kilimanjaro.
Wakati huo huo, mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam walijitokeza kwa wingi hospitalini hapo kuuaga mwili wa Anthery.
Mushi
aliendelea kufafanua kuwa hakuna mtu anayejua hasa kuhusu nini siri ya
ugomvi wao mpaka sasa, zaidi ya kufahamu kuwa ndugu yao alirudi kimya
kimya, na kwenda Uru mkoani Kilimanjaro kabla ya kurudi jijini Dar es
Salaam siku ya Jumamosi.
Mushi alisema kuwa ulitokea ugomvi kati yake na mzazi mwenzie na wakaamua kwenda kwa mama yake, Ufoo ili kuusuluhisha.
Alisema
kulitokea kutokuelewana kulikosababisha Anthery achukue maamuzi magumu
ya kumpiga risasi mkwe wake, Anastazia Saro na kumuua hapo hapo na
kumpiga risasi mbili mzazi mwenzie, Ufoo Saro na kisha kuchukua maamuzi
magumu ya kujiua yeye mwenyewe kwa kujipiga risasi.
Alisema tukio hilo limeleta mshtuko mkubwa na simanzi katika familia yao, kwani Anthery alikuwa ni mtu mpole na mkimya sana.
No comments:
Post a Comment