Kwa mujibu wa Ommy Dimpoz, show za nyumbani ndizo zinazolipa zaidi, kuliko zile za nje ya nchi.
Ommy alikuwa akiongea na kipindi cha Ampilifaya jana baada ya kurejea kutoka nchini Marekani alikokuwa kwenye ziara ya wiki tatu.
“Naweza kusema hapa nyumbani tunalipwa hela nyingi kuliko tunavyopata nje kwa msanii yeyote kwa asilimia kubwa. Inategemea pia unaenda kufanya tamasha sehemu gani. Kwahiyo asilimia kubwa hela unatengeneza zaidi nyumbani,”alisema Ommy.
Alisema hiyo ni kwasababu show za Tanzania huhudhuriwa na watu wengi zaidi kuliko inavyokuwa nchi za nje ambako ni watu wachache sana huingia japo kiingilio ni kikubwa na wengi wanaohudhuria ni watu waliotoka Afrika Mashariki zaidi.
Katika hatua nyingine, leo Ommy Dimpoz kupitia Instagram, ameandika maneno ya shukrani kwa wote walioifanikisha show yake.
“AssaLaam ALeykum Ndugu zangu,Eid MubaraQ Ndugu,jamaa,Marafiki,and all my Fans all over the world…Namshukuru mungu Alhamdulilah nimerudi nyumbani Salama Kuendelea na Majukumu mengine baada ya Tour ya Takriban Mwezi Mmoja…Ningependa kuchukua Nafasi hii kuwashukuru @Dmkglobalpromotion na J&P kwa kufanikisha tour yangu ambayo imeweza kuwa na Mafanikio makubwa Na kufanikisha baadhi ya malengo ambayo mengine sikuyatarajia.Pia ningependa kuwashukuru watu wote ambao walionyesha support kipindi chote cha tour yangu hususan Watanzania wenzangu na Watu wa Africa Mashariki na Kati ambao walionyesha Ushirikiano na support ya kutosha tangia mwanzo mpaka mwisho wa tour yangu…Nachoweza kuwaahidi ni kuwa mengi mazuri Yanakuja na Naimani sitawaangusha.Nawatakia mapumziko na sherehe njema za sikukuu ya Idd….Mimi na team nzima ya pozkwapoz tutakuwa DARLIVE tukitoa Huduma Karibuni sana.LOVE U ALL.”
-Bongo5

No comments:
Post a Comment