Taarifa ya uamuzi huo imetolewa leo kwenye mkutano wa makadinali unaoendelea mjini Vatican, ikiwa ni hatua mihimu ya kuthibitisha tangazo lake la Julai mwaka huu kwamba atawapa heshima viongozi hao wawili wa juu wa Kanisa waliopita katika karne ya 20.
Wachambuzi wa masuala ya Kanisa hilo alieleza kwamba inaonekana umuzi huo ni wa makusudi ikiwa ni hatua ya kujaribu kuliunganisha kanisa hilo ambalo lina mkanganyiko kwa sasa.
Kila mmoja ana watu wanaomuunga mkono na wanaompinga, ambapo kwa sasa Francis anaonekana kuungwa mkono na wote wa pande zote mbili hivyo kuwa kichocheo cha kuunganisha na kufuta makovu yaliyolikumba Kanisa hilo kwa miaka ya hivi karibuni
No comments:
Post a Comment