Madereva
na Mafundi wa Treni za TAZARA wakiwa katika moja ya vichwa sita vipya
vya Treni ambavyo vimeletwa Tanzania na wapo katika mafunzo ya jinsi ya
kuvitumia. (Picha na Furaha Eliab, Mbeya)
Na Furaha Eliab, Mbeya
SHIRIKA
la reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) limepata vichwa sita vya Treni
vipya kutoka nchini China vyenye uwezo wa kubeba tani 1800 kila kimoja.
Kufuatia
kutolewa kwa vichwa hivyo vya Treni vipya, madereva 160 na mafundi 80
wa karakana ya Treni Iyunga mkoani Mbeya wanapatiwa mafunzo yakakayo
wawezesha kufanya kazi kwa umakini katika vichwa hivyo.
Akitoa
maelezo ya ujio wa vyicho hivyo Mhandisi Mwandamizi katika karakana na
Iyunga Eng. Davie Tembo alisema kuwa vichwa hivyo vya treni vyenye
uwezzo wa kubeba Tani 1800 vimeletwa Juzi katika karakana hiyo.
Alisema
kuwa vimetoka nchini china na ni toleo jipya ambalo linahitaji madereva
na mafundi kujifunza kabla ya kuanza kutumia kwani linatumia mfumo
mpya.
Tembo
alisema kuwa kampuni ya CSR Qishuyan ya nchini China ndio iliyo
tengeneza vichwa hivyo na inatoa mafunzo kwa madereva na mafundi jinsi
ya kuvimudu vichwa hivyo.
Alisema kuwa wamevijaribu vichwa hivyo na kuviona vinafaa kwa matumizi na havina shida yoyote.
Awali
akifungua mafunzo kwa madereva hao Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA,
Said Sauko alisema kuwa mafunzo hayo yatalenga kwa Wafanyakazi wa
TAZARA watakao kuwa katika makundi saba ambapo kila kundi litakuwa na
watu wasio pungua 40.
Alisema kuwa mafunzo hayo yatatolewa kwa muda wa mwezi mmoja na yamelenga kwa wafanyakazi kutoka Tanzania na Zambia.
No comments:
Post a Comment