Wanafunzi
wa Shule ya Viziwi Dongobesh wakiimba wimbo wa Taifa shuleni hapo
mkoani Manyara. Kukosekana kwa walimu wa kufundisha lugha ya alama,
imesababisha wanafunzi 39 kati ya 40 wenye ulemavu wa kutosikia
waliomaliza elimu ya sekondari mwaka jana kupata daraja sifuri.
Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria, Jasmine-Angellah Kairuki, amesema kukosekana
kwa walimu wa kufundisha lugha ya alama, imesababisha wanafunzi 39 kati
ya 40 wenye ulemavu wa kutosikia waliomaliza elimu ya sekondari mwaka
jana kupata daraja la sifuri.
Akizungumza
Dar es Salaam juzi, Kairuki alisema changamoto zinazowakabili watu
wenye ulemavu huo kwa elimu ni kutokuwa na fursa sawa ya kutumia lugha
wanayomudu.
Alisema
utoaji elimu kwa watu wenye ulemavu huo, hauridhishi kutokana na walimu
waliopo kuwa wachache ndiyo maana wanafunzi 39 walifeli na mmoja kupata
daraja la nne.
"Tatizo
hili linatokana na walimu wanaofundisha lugha ya alama kuwa wachahe,
hivyo nakuagiza Kamishna wa Idara ya Ustawi wa Jamii kutembelea shule za
wanafunzi wasiosikia kuangalia elimu yao inatolewaje ili tupunguze
tatizo lililopo," alisema Kairuki.
Kaiuiki
alisema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wataendelea
kuelimisha jamii, ili kupata haki haki zao wanazostahili ikiwamo fursa
ya kutumia lugha ya alama kuanzia shule ya msingi hadi sekondari.
Ofisa
Uhusiano wa Umoja wa Miradi Chama cha Viziwi Tanzania (Chavita), Tungi
Mwanjalu, alisema hali hiyo inatokana na kukosekana kwa walimu wenye
ujuzi wa kutumia lugha ya alama na kubuni nyezo rahisi za kufundishia
viziwi.
Mwanjalu
alisema kutokana na tatizo hilo, viziwi nchini hawana ajira na kushindwa
kudai haki zao za msingi ndani ya jamii inayowazunguka na kuonekana ni
mzigo kwa taifa.
No comments:
Post a Comment