Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, October 3, 2013

UTUMISHI YAIPA KIPIGO TAKATIFU TAMISEMI,YATINGA NUSU FAINALI SHIMIWI


IMG_3301Timu ya mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais, Menejmenti ya Utumishi wa Umma ”Kombani queens” ikifanya mazoezi mepesi kabla ya kuingia uwanjani kupambana na  TAMISEMI katika mashindano ya SHIMIWI Kiwanja cha Jamhuri mjini Dodoma hizi ni taswira za timu ya mpira wa Pete ya Utumishi “Kombani Queens” ilipoingia fainali kwa kuikung’uta TAMISEMI katika michezo ya SHIMIWI inayoendelea. Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ‘Kombani queens” imeshinda mpambnano huo kwa goli  38-28 na kuingia nusu fainali.
IMG_3305 Timu ya mpira wa Pete ya TAMISEMI  ikifanya mazoezi kabla ya kupambana wenzao wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma “Kombani Queens” . IMG_3307Timu ya mpira wa Pete ya TAMISEMI ikisalimiana na timu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma “Kombani Queens” kuashiria mwanzo wa mpambano wao wa Mpira wa Pete kuwania kuingia nusu Fainali za SHIMIWI. IMG_3324Mchezaji wa timu ya mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma “Kombani queens”  Monica Aloyce (GK) (aliyeruka juu) akiondoa hatari kutoka kwa wachezaji wa timu ya  TAMISEMI wakati wa mpambano dhidi ya timu hizo. IMG_3349Mchezaji wa timu ya mpira wa Pete ya TAMISEMI Defroza Otilia (GA) akijaribu kutoa pasi wakati wa mpambano na Utumishi  mjini Dodoma, mbele yake akikabwa na mchezaji wa Utumishi Monica Aloyce (GK) . IMG_3364Mchezaji wa timu ya mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ”Kombani queens” Elizabeth Fussi (C) akitoa pasi wakati wa mpambano dhidi ya TAMISEMI  katika mashindano ya SHIMIWI mjini Dodoma. Mbele yake ni mchezaji wa TAMISEMI Imelda Hango (C) akijaribu kumzuia .
IMG_3365Fatma Ahmed (GS) wa timu ya mpira wa Pete ya ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  akichukua pasi kutoka kwa Anna Msulwa (GA) (aliye mbele yake) katika mashindano ya SHIMIWI mjini Dodoma. Utumishi iliifunga TAMISEMI mabao 38-28.

No comments:

Post a Comment