MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), AbsalomKibanda,akiwa na mchezaji wa wanahabari Iringa Lukelo Mkami
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), AbsalomKibanda,
kulia akiwa na wachezaji wa timu zote mbili kabla ya mchezo na
kushoto ni mwalimu wa timu ya jukwaa la wahariri Bw Masoud
Mzee
wa matukio daima jezi nnamba 7 akiwajibika uwanjani baada ya
kuingia kipindi cha pili huku mwamuzi wa mchezo huo Frederick
Mwakarebela kushoto akikimbia kuufuata mpira
Washambuliaji
hatari mzee wa matukio daima namba 7 ,mbunge Msigwa namba 2 kushoto
na Raymond Francis mwenye rasta wakiwajibika vema
………………………………………………………………………….
Na Francis Godwin BlogTIMU
ya jukwaa la wahariri wa habari Tanzania (TEF) imekuwa ni sawa na
sikio la kufa ambalo kamwe halisikii dawa baada ya kukubali kupokea
tiba ya bakora moja kutoka kwa wanahabari mkoa wa Iringa .
katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Samora Iringa jana ,mchezo uliojaa vionjo vya kila aina kutoka kwa timu zote mbili pamoja na mwamuzi wa mchezo huo aliyekuwa katibu mkuu wa TFF Frederick Mwakalebela timu hizo ziliweza kuvunja mbavu za mashabiki uwanjani hapo.
Wakati wachezaji wa timu ya wanahabari Iringa baada yao wakionyesha kujikata chenga wenyewe kwa wenyewe ,timu ya jukwaa ambayo ilikuwa na wachezaji waliokula chumvi nyingi huku baada yao wakishindwa kukimbia kutokana na vitambi walivyokuwa navyo bado kipindi cha kwanza kilimalizika bila ya timu hizo kuona nyavu ya mwingine.
kipindi cha pili timu zote vilifanya mabadiliko makubwa zaidi kwa kuwatoa wachezaji karibu ya nusu ya wali waliocheza kipindi cha kwanza na kuweka wapya hali iliyoonekana ni ngumu zaidi kwa jukwaa la wahariri na nyepesi kuliko kwa wanahabari Iringa ambao waliweza kutumia mabadiliko hayo kuwacharaza bakora wahariri hao .
Wanahabari Iringa wakicheza kwa nguvu zote kipindi cha pili walipata bao la kuongoza na kufungia dimba dakika ya 3 kipindi cha pili goli lililodumu hadi mwisho wa mchezo huo.

Awali
katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo (TASWA) mkoa wa
Iringa Francis Godwin alisema kuwa mbali ya timu yake kushinda
ila ushindi huo ni mwembamba sana na kuwa walipendezewa kuichapa
timu hiyo ya jukwaa la wahariri kwa jumla ya magoli 5-0.
Hata
hivyo aliwashukuru wadhamini wa mchezo huo ikiwemo kampuni ya simu ya
Voda Com kwa kudhamini mchezo huo kwa asilimia 100 ,mdau wa michezo
mkoa wa Iringa Frederick Mwakalebela aliyetoa zawadi ya ng’ombe kwa
mabingwa wa mchezo huo timu ya wanahabari mkoa wa Iringa pamoja na
jukwaa la wahariri kwa kuamua kuja kucheza na wanahabari mkoa wa
Iringa.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika mchezo huo mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda alisema kuwa mbali ya timu yake kufungwa ila bado wanahabari Iringa wameonyesha ushirikiano mkubwa kwa wahariri hao.
Kwani alisema kuwa jukwaa la wahariri kila mwaka limekuwa na mkutano mkuu wa mwaka na kufanyika katika mikoa mbali mbali na mwaka huu wamechagua Iringa kuja kufanya mkutano wao na kucheza mchezo huo wa kirafiki na wanahabari wa mkoa wa Iringa.

No comments:
Post a Comment