Pages

Sunday, October 27, 2013

WAHARIRI TANZANIA WACHARAZA, WAPEWA DOZI YA BAKORA NA WANAHABARI IRINGA

 MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), AbsalomKibanda,akiwa na mchezaji wa wanahabari Iringa Lukelo Mkami
 
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), AbsalomKibanda, kulia akiwa na  wachezaji wa  timu  zote  mbili kabla ya mchezo na kushoto ni mwalimu wa  timu ya jukwaa la  wahariri Bw Masoud
 Mzee  wa matukio  daima jezi nnamba  7 akiwajibika  uwanjani baada ya  kuingia  kipindi  cha pili  huku mwamuzi wa mchezo huo Frederick Mwakarebela kushoto akikimbia kuufuata mpira
 Washambuliaji hatari mzee  wa matukio  daima namba 7  ,mbunge Msigwa namba 2 kushoto na Raymond Francis mwenye rasta  wakiwajibika vema
………………………………………………………………………….
Na  Francis Godwin BlogTIMU  ya  jukwaa la  wahariri  wa habari Tanzania (TEF) imekuwa ni  sawa na sikio la kufa ambalo kamwe  halisikii  dawa baada ya  kukubali kupokea  tiba ya bakora  moja kutoka kwa wanahabari  mkoa  wa Iringa .

katika  mchezo  huo uliochezwa katika uwanja  wa Samora Iringa jana ,mchezo uliojaa vionjo  vya kila aina kutoka kwa timu  zote mbili pamoja na mwamuzi wa mchezo huo aliyekuwa katibu mkuu wa TFF Frederick Mwakalebela timu  hizo ziliweza  kuvunja mbavu  za mashabiki uwanjani hapo.

Wakati wachezaji wa  timu ya  wanahabari Iringa baada yao  wakionyesha  kujikata  chenga  wenyewe kwa  wenyewe ,timu ya jukwaa ambayo ilikuwa na wachezaji waliokula  chumvi nyingi  huku baada yao  wakishindwa  kukimbia kutokana na vitambi walivyokuwa navyo bado kipindi cha kwanza  kilimalizika bila ya timu  hizo  kuona nyavu ya mwingine.

kipindi  cha  pili  timu  zote  vilifanya mabadiliko makubwa  zaidi kwa  kuwatoa  wachezaji karibu ya nusu  ya  wali  waliocheza kipindi cha kwanza na kuweka wapya hali  iliyoonekana ni ngumu  zaidi kwa jukwaa la  wahariri na nyepesi kuliko kwa wanahabari Iringa ambao  waliweza  kutumia mabadiliko hayo  kuwacharaza bakora wahariri  hao .

Wanahabari  Iringa wakicheza kwa nguvu zote kipindi cha pili walipata  bao la kuongoza na kufungia  dimba  dakika ya 3  kipindi  cha pili goli  lililodumu hadi mwisho  wa mchezo huo.
Awali katibu  wa chama cha waandishi  wa habari  za michezo (TASWA) mkoa  wa Iringa  Francis Godwin alisema  kuwa mbali ya  timu  yake  kushinda  ila  ushindi  huo ni mwembamba sana na kuwa  walipendezewa kuichapa  timu  hiyo ya  jukwaa la  wahariri kwa jumla ya magoli 5-0.
Hata  hivyo aliwashukuru wadhamini wa mchezo  huo ikiwemo kampuni ya simu ya Voda Com kwa  kudhamini mchezo huo kwa asilimia 100 ,mdau wa michezo  mkoa  wa Iringa Frederick Mwakalebela aliyetoa  zawadi ya ng’ombe kwa mabingwa wa mchezo huo  timu ya wanahabari  mkoa  wa Iringa pamoja na jukwaa la wahariri kwa kuamua  kuja  kucheza na wanahabari mkoa wa Iringa.

Kwa  upande  wake mgeni rasmi katika mchezo huo mwenyekiti  wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda alisema  kuwa mbali ya  timu yake kufungwa ila bado wanahabari Iringa  wameonyesha ushirikiano mkubwa kwa  wahariri hao.

Kwani  alisema  kuwa jukwaa la  wahariri  kila mwaka  limekuwa na mkutano mkuu wa mwaka na kufanyika katika mikoa mbali mbali na mwaka  huu  wamechagua Iringa kuja kufanya mkutano  wao na kucheza mchezo  huo wa kirafiki na  wanahabari wa mkoa  wa Iringa.

No comments:

Post a Comment