Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, October 4, 2013

WATUHUMIWA WA MAUAJI YA BILIONEA MSUYA WAFIKISHWA MAHAKAMANI TAZAMA PICHA




WATUHUMIWA wa mauaji ya mfanyabiashara wa madini ya tanzanite, Erasto Msuya (43) wakiwemo wafanyabiashara maarufu wa madini hayo, Joseph Damas “Chusa” na Sharif Mohamed Athuman wote wakazi wa Jiji la Arusha jana wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Moshi.
Watuhumiwa hao wote kwa pamoja walifikishwa mahakamni hapo wakiwa katika gari maalumu la kubeba watuhumiwa majira ya saa 5:30 asubuhi wakiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi wenye silaha, wakiwemo wa kikosi maalumu cha kutuliza ghasia (FFU).
katika chumba cha mahakama kilichowezesha watu wachache kuingia ndani, mwendesha mashitaka wa serikali, wakili Stella Majaliwa baada ya kutaja makosa yanayowakabili washitakiwa aliomba kuahirishwa kwa kesi hiyo kutokana na kutokamilika kwa upelelezi.


Wakili Stella aliieleza mahakama hiyo kuwa washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kutokana na kesi ya mauaji ya kukusudia kinyume na kanuni namba 16, kifungu cha 196 ya sheria za makosa ya jinai.


Kutokana na ombi hilo, hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu mkazi Simon Kobelo aliridhia na kupanga tarehe nyingine.


Kesi hiyo sasa itatajwa tena Oktoba 15 mwaka huu wakati washitakiwa wote wamerudishwa mahabusu. Mara ya kwanza washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Agosti 21, mwaka huu.


Wahitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Shaibu Mpungi, Musa Mangu, Jalila Zuberi, Sadiki Jabiri na Joseph Mwakipasile.


Mfanyabiashara Erasto Msuya aliuawa Agosti 7, mwaka huu majira ya 6:30 mchana kwa kupigwa risasi 13 kifuani, kando ya barabara kuu ya Arusha – Moshi katika eneo la Mjohoroni, Wilaya ya Hai, karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).





Watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabishara wa madini ya Tanzanite jijini Arusha,Erasto Msuya wakifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment