Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, November 26, 2013

ABDULRAHMAN KINANA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA RUNGWE MASHARIKI


1 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata mbao kwa ajili ya kupiga Kenchi za bati wakati aliposhiriki ujenzi wa shule ya sekondari ya Mwakaleli Wilayani Rungwe katika mkoa wa Mbeya, wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo, huku akikagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha Mapinduzi na uhai wa chama, Katika ziara hiyo Kinana ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi na Dr.Asha Rose  Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa kiamataifa , leo Ndugu Abdulrahman Kinana alikuwa katika jimbo la Rungwe Mashariki linaloogozwa na Profesa Marck Mwandosya, kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Sombyo Ivestiment. 2 Dr.Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa kiamataifa akikata mbao kwa ajili ya kupaua jengo la maabara katika shule sekondari ya Mwakaleli wanaoshuhudia kutoka kulia ni Nape Nnauye katibu wa NEC Itikadi na uenezi, Mkuu wa wilaya ya Rungwe Bw. Crispin Meela,Mkurugenzi wa kampuni ya Sombyo Inestmaent na kushoto ni Mwenkiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Godfrey Zambi. 3Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Mkuu wa shule ya sekondari ya Mwakaleli Bw. Edward Mwantimwa wakati akikagua ujenzi wa jengo la maabara shuleni hapo leo.
4Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipandisha tofali juu kwa ajili ya ujenzi wa jengo la maabara katika shule ya sekondari ya Mwakaleli. 5Kinana akibeba tofari wakati aliposhiriki ujenzi wa nyumba ya mwalimu katika shule ya sekondari ya Mwakaleli wilayani Rungwe. 6Mkuu wa wilaya ya Rungwe Bw. Crispin Meela akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mwakaleli. 7Dr.Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa kiamataifa akizungumza jambo na wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari ya Mwakaleli. 9Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akiwaasa jambo wanafunzi wa sekondari hiyo 10Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki Mh Godfrey Zambi 11Kinana akizungumza na wananchi wanafunzi huku akiwa karibu na Mkuu wa shule hiyo Bw. Edward Mwantimwa 12Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Mbunge wa viti maalum mkoani Mbeya wakipiga picha ya pamoja na wanafunzi wa shule hiyo 13Wazee wa kinyakyusa wakicheza mgoma wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Kandete 14Kada wa Chama cha Mapinduzi Bw, Richard Kasesela akichezo ngoma ya Kinyakyusa 16Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa akizungumza na wana Kandetea . 18Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi akizungumza na wananchi katika kata ya Kandete. 19Wazee wa Kandete wakimsikiliza Nape Nnauye. 20Katibu wa Itikadi, Siasa na UenChief Mwakinana kama alivypewa na Wazee wa Kandete 21Dr. Asha Rose Migiro akiwa amekaa kwenye mkeka baada ya wanawake wa Kandete kumpatia zawadi ya kitenge 22Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa Kandete leo.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-RUNGWE MASHARIKI
 

No comments:

Post a Comment