Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, November 29, 2013

Brandts afyeka watano Yanga, Bahanuzi agoma


Khatimu Naheka na Hans Mloli
KOCHA Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts ameweka wazi kuwa katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo, atapunguza wachezaji watano kwa kutolewa kwa mkopo.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Brandts alisema kwa sasa kikosi chake kina jumla ya wachezaji 30 ambapo anataka kupunguza idadi hiyo kwa kuwatoa kwa mkopo watano.
Kocha huyo raia wa Uholanzi ameeleza kuwa, lengo lake ni kuwa na kikosi chenye wachezaji 25 kwa lengo la kupunguza gharama za uendeshaji.
Alipotakiwa kuwataja wachezaji hao, kocha huyo aligoma kuwataja kwa majina, ingawa Championi Ijumaa lina uhakika kuwa, baadhi ya wachezaji hao ni; Said Bahanuzi, Shaban Kondo, Hussein Javu na Ibrahim Job.
“Nataka kupunguza idadi ya wachezaji katika timu, tayari hilo nimeshazungumza na uongozi, kama unataka kufahamu zaidi waulize viongozi,” alisema.
Akizungumza na gazeti hili juu ya kutolewa kwa mkopo, Bahanuzi alisema: “Sipo tayari kutolewa kwa mkopo, bora nibaki nilale nyumbani mpaka mkataba wangu utakapokwisha, kama Yanga hawanitaki bora niwe huru tu, mkopo ambao naweza kwenda ni wa Simba au Mtibwa Sugar.”chanzo GPL



No comments:

Post a Comment