Kitila Mkumbo
Tunawashukuru
watanzania kwa kufuatilia kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Nawapa pole
wote waliokwazwa na jambo hili, na ninawashukuru wote walionipa pole na
kunitia moyo. Ninawashukuru pia walionilaumu na ni vizuri kunyosheana
vidole na kuwekana sawa pale ambapo moja wetu anaonekana kukwamisha
harakati za mabadiliko.
Haya
ni mawimbi katika harakati za mabadiliko na ninaamini yatapita na
hayatayumbisha mchakato wa kusimika mfumo wa demokrasia hapa nchini
kwetu.
Ninashauri
tuwe na subira katika kutoa hitimisho na hukumu katika jambo hili.
Mpaka sasa tumekwisha kupata upande mmoja juu ya kilichotokea. Vuteni
subira nasi tuseme ndipo mpitishe hukumu. Mungu akijalia tutakuwa na
mkutano na waandishi wa habari wakati wowote kabla ya wiki ijayo na
tutaeleza upande wetu, na hasa kutoa maoni yetu juu ya kile
kilichotamkwa jana kwamba sisi ni wahaini na wahujumu ndani ya chama
chetu.
Kwa sasa
tambueni tu kuwa mie binafsi bado nipo imara katika kuhakikisha kwamba
siwi kikwazo na ninachangia kikamilifu nguvu zangu katika harakati
takatifu za mabadiliko hapa nchini.
No comments:
Post a Comment