Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, November 28, 2013

Exclusive: Roma aitolea maelezo tweet inayoaminika kumdisi Kimbunga, 'Ukikosa shukrani kama Kimbunga, utaishia kugongea weed'



Rapper anawakilisha mkoa wa Tanga, Roma Mkatoliki ameitolea maelezo tweet yake ya leo (November 28) ambayo ilionekana kuwa ilikuwa inamdiss rapper Kimbunga ambaye alimvaa Roma kwenye ngoma yake ‘Natuma Salaam’.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, Roma amesema kuwa tweet hiyo imebeba mashairi ya ngoma yake aliyoifanya muda mrefu uliopita lakini bado haijasikika.
“Hiyo ni mistari ambayo imeandikwa katika akaunti yangu ya Twitter na Facebook ni mojawapo ya mistari ya ngoma zangu ambazo zimesharekodiwa muda mrefu tu. Ni ngoma ambayo haijawahi kusikika katika stock ya Roma, ni kama ambavyo nilikuwa naweka mistari ya Mathematics, Tanzania na ngoma nyingine ambazo nilikuwa naweka.” Roma ameiambia tovuti ya Times Fm.
 Kuhusu mstari unaotaja Kimbunga ambaye aliwahi kufanya nae ngoma inayoitwa ‘Nawarudisha kwao’, Roma alifunguka.
  R.O.M.A @Roma_Mkatoliki
Ukikosa shukrani kama kimbunga, utaishia kugongea weed/ Kama ustaadh anayengoja mpunga au maandazi ya maulid/ Rooooma!! 12/12/2013!!

“Ni mapema sana kuelezea lakini inawezekana ni ‘kimbunga’ upepo ule ambao tumeuzoea. Kimbunga artist si ni mwana familia wa Tongwe kila siku tuko nae kila siku. Ni msanii ambaye nilishawahi kufanya nae ngoma inaitwa ‘Nawarudisha Kwao’, Kimbunga featuring Roma, Jose mtambo na Domo Kaya.
“Lakini tuichukulie tu kabisa kwamba ukikosa shukurani kama kimbunga utaishia kugongea weed, weed kila mtu anaijua na kimbunga kila mtu anakijua ni kaka yake ama dada yake upepo. Na tunajua weed inaendana na hali ipi ya upepo, kama ni Kimbunga ama Katrina. So, I’m sure siku ngoma ikitoka itakuwa wasaa mzuri wa kuongea na kuelezea zaidi kuhusu hiyo ngoma.”Amefafanua Roma Mkatoliki.
Ameongeza kuwa December 12 ni siku yake ya kuzaliwa kwa hiyo siku hiyo atafanya kitu kikubwa kwa familia yake na fans wake. 
“December 12 ni siku yangu ya kuzaliwa ambayo mara ya kwanza huwa napenda kushare kitu na familia, maisha yangu binafsi au muziki. Mwaka jana ilikua itoke 2030 siku hiyo lakini ikatokea changes flani ikachelewa kutoka na ikatoka December 29. So, mwaka huu lazima kuna kitu chochote ntakifanya kwa ajili ya familia yangu na fans wangu. Ni mapema sana kusema lakini December 12 ni siku yangu ya kuzaliwa, ijulikane hivyo na kuna kitu chochote kinaweza kufanyika.”Amefunguka Roma.
Unaweza kuifuatilia story hii zaidi kupitia ‘The Jump Off’ na ‘Bongo Dot Home’ ya 100.5 Times Fm.



No comments:

Post a Comment