ALLY OMARY CHITANDA MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA LINDI
30/11/2013 KATIBU WA CHADEMA
MKOA WA LINDI
YAH; KUJIUZURU UENYEKITI WA MKOA
Somo la hapo juu lahusika.
Napenda kuchukua nafasi hii kukuarifu kuwa kwa hiari yangu bila ya kushawishiwa na mtu yeyote, nimeamua kujiuzuru nafasi ya Uenyekiti wa Mkoa tangu leo tarehe 30/11/2013.
Nashukuru sana kwa ushirikiano wako pamoja na Viongozi wote wa Baraza la Uongozi pamoja na Baraza la Mashauriano la Mkoa, lakini pia niwashukuru Viongozi wote wa Majimbo naWilaya hasa Nachingwea ambao kwa kiasi kikubwa, wameniwezesha kufika hapa hasa wakati mgumu wa Ujenzi wa Chama na kugombea Ubunge 2005 na 2010.Matarajio yangu ya kuweza kukomboa wanyonge kupitia CHADEMA kwa sasa sioni kama yanaweza kufikika.
Nitabaki kuwa Mwanachama wa kawaida na ninaahidi kuwa Mwanachama mwaminifu na pale nitakapohitajika nikotayari kusaidiana na Viongozi kujenga Chama.Nawataki kazi njema na Ujenzi wa Chama.
Ahsante kwa ushirikiano.
………………………………..
A.O. CHITANDA
CHANZO GPL
No comments:
Post a Comment