Hali ya
afya ya Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi
aliyelazwa katika Hospitali ya Millpark nchini Afrika Kusini inaelezwa
kuwa ni mahututi.
Mbunge
wa Kuteuliwa, James Mbatia akizungumza jana bungeni mjini Dodoma wakati
akichangia Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Katiba
alisema, kutokana na hali ya mjumbe huyo kuwa mbaya, aliwaomba
Watanzania kuendelea na sala kwa ajili yake.
Mbatia
alisema, “Kwa kuwa tunazungumzia suala la katiba huku mmoja wa wajumbe
wake Dk Mvungi ni mgonjwa, tunahitaji kufanya mchakato huu kwa kuweka
mbele masilahi ya taifa.
“Hali yake
Dk Mvungi bado ni mbaya sana huko katika hospitali ya Millpark na
anahitaji kuombewa, hivyo Watanzania wote tumwombee,” alisema Mbatia
ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi.
Daktari
wa kitengo hicho ambaye hakutaka kuweka wazi jina lake alisema,
wanaendelea kufanya kila mbinu za kitaaluma ili kuokoa maisha ya
Mtanzania huyo.
“Tunafanya kila tuwezalo kumwondoa katika hali hii kwa sababu ameumia zaidi katika mishipa ya fahamu. Tunajitahidi,” alisema.
Msemaji
wa Wizara ya Afya, Nsachris Mwamaja alisema wizara inafuatilia kwa
ukaribu maendeleo ya Dk Mvungi ingawa hawezi kusema chochote kwani suala
hilo lipo mikononi mwa familia.
No comments:
Post a Comment