Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, November 28, 2013

Huyu ndio mrembo wa Kitanzania alietangazwa mshindi wa taji la “Miss Commonwealth Africa” huko London Uingereza


The crowned queens of the Commonwealth 2013-pic by Jay PedramMtanzania, Malkia Kassu ( wa tatu toka kushoto) akiwa na washindi wenzake – wote wamevalia taji na kubeba vikombe vya ushindi.
Mashindano ya 2013 yalifanyika London Jumamosi Novemba 26 na  kwa mara ya kwanza yalikuwa na mshiriki toka  Tanzania.
Malkia Kassu (  jina la kuzaliwa Mulki Kassu  Miraj) alichaguliwa malkia wa Tanzania na  bara zima la Afrika.
Wateuzi wa ushindi huo hawakuangalia tu sura,  bali tabia, fikra, hamasa na msimamo wa kimaendeleo wa mhusika ambapo washindani walitoka mataifa mbalimbali duniani.
“Ninataka kuiwakilisha nchi yangu na kuwasaidia wenye maisha magumu, niifanye dunia iwe mahali pazuri zaidi. Nafahamu si kazi rahisi ila nina hakika kila mmoja wetu akijumuika na mwenzake  mabadiliko mema zaidi yatafanyika. Tanzania ni nchi ya amani na ninaamini amani na mapenzi vyaweza kuongezeka katika jumuiya zetu.” – Kassu
 Ali Sungura-mdhamini, Balozi Kallaghe, Malkia Kassu, Aisha Mohammed, Allen Kuzilwa- London 2013- pic by Said SururKutoka kushoto ni mdhamini, Ali Sungura, Balozi wa Tanzania Uingereza , mheshimiwa Peter Kallaghe,  Aisha Mohammed na Afisa Ubalozi Allen Kuzilwa
Malkia Kassu -2013Malkia Kassu
Malkia Kassu with pals Andrew Matt and Ayesha Mohammed-pic by Jay PedramMalkia Kassu akipongezwa na marafiki, Andrew Matt na Aisha Mohammed. Malkia with Diamond the Tanzanian star musician- 2013-pic by Kassu familyMalkia Kassu akiwa na mwanamuziki maarufu wa Bongo Fleva, Diamond karibuni.
Winner Malkia Kassu with friends Ayesha Mohammed and Andrew Matt 
Stori imeandaliwa na Frank Eyembe.


No comments:

Post a Comment