Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, November 28, 2013

WAZIRI MKUU AONGOZA MAZISHI YA ASKOFU SIMALENGA

PG4A6916Waziri Mkuu, Mizengo pinda akisalimiana na Maaskofu wa kanisa la Anglican nchini wakati alipowasili kwenye kanisa kuu la Anglican la Njombe kuhudhuria mazishi ya Askofu wa Dayosisi  ya South West Tanganyika, , John  Andrew Simalenga Novemba 28, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A6943 Waziri Mkuu, Mizengo Pindaakitoa heshima za mwisho kwa Askofu John Andrew Simalenga katika mazishi ya Askofu huyo wa Dayosisi ya South West Tanganyika ya Kanisa la Anglican lyaliyofanyika Njombe  Novemba 28, 2013.  Kushoto ni Askofu Mkuu wa kanisa la Anglican nchini, Dr. Jacob  Chimeledya.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A6971Mwili wa Askofu wa Kanisa la Anlican Dayosisi  ya Southa  west, John Andrew Simalenga  ukitelemshwa kaburini kwenye mazishi yaliyofanyika wenye kanisa kuu la  Dayosisi hiyo mjini Njombe Novemba 28, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A6996Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka mchanga katika kaburi la Askofu wa Dayosisi  ya  South West Tanganyika ya Kanisa la Anglican, John Andrew Simalenga yaliyofanyika  mjini Njombe Novemba 28, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A7095Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika ibada ya mazishi ya Askofu wa Kanisa  la Anglican Dayosisi ya South West Tanganyika , John Andrew Simalenga yaliyofanyika Njombe Novemba 28, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A7045Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiweka shada la maua kwenye kaburi la Askofu wa Dayosisi ya South West Tanganyika , John Andrew Simalenga  katika mazishi yaliyofanyika Njombe Novemba 28, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameongoza mamia ya watu kwenye ibada ya
mazishi ya Askofu wa Saba wa Dayosisi ya South West Tanganyika ya
Kanisa la Anglikana Tanzania Mhashamu Askofu John Andrea Simalengailiyofanyika Njombe mjini.
Akizungumza na mamia ya waumini na waombolezaji waliohudhuria ibada hiyo ya mazishi leo mchana (Alhamisi, Novemba 28, 2013) Waziri Mkuu alisema Dayosisi hiyo imepoteza mhimili muhimu lakini akawataka wawe na umoja na upendo huku wakiendelea kumtumainia Mungu.
“Mhashamu Baba Askofu Simalenga alisimikwa Julai 6, 2008. Ni miaka mitano tu ya utumishi kwenu na alikuja wakati ambapo Dayosisi hi ilikuwa imekaa kwa miaka 10 bila ya kuwa na kiongozi. Siku anawekwa wakfu nilikuwepo na ninakumbuka mlimuomba asaidie kuleta mshikamano,” alisema Waziri Mkuu.
“Ninawaomba wanadayosisi muwe na upendo na mshikamano mkubwa miongoni mwenu hadi hapo Mungu atakapotupatia kiongozi mwingine. Tumuombe Mungu ili kiongozi huyu ajaye apatikane kwa njia ya amani,” alisisitiza.
Alimuomba mke wa marehemu, Bibi Martha pamoja na watoto wa marehemu waupokee msiba huo kwa mikono miwili na kuahidi kuwaombea faraja kwa Mwenyezi Mungu.
Waziri Mkuu ambaye alishiriki mazishi hayo kwa niaba ya Serikali, alitumia fursa hiyo kuwapa pole maaskofu, mapadri, watawa na familia zikiwa ni salamu maalum kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye alisema yuko ziarani kwenye mkoa mpya wa Simiyu.
Naye Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bibi Anne Makinda ambaye pia ni mbunge wa Njombe Kusini ilipo Dayosisi hiyo akitoa salamu za rambirambi alisema wana Njombe wamepungukiwa na nguvu kwa kuondokewa na Askofu Simalenga.
“Alisaidia kuleta umoja hapa kwetu, tumempoteza mtu muhimu sana katika harakati za maendeleo ya wilaya yetu na mkoa kwa ujumla. Alisaidia kuleta umoja na upendo na sisi tuwe na upendo na amani, tuendelee kumuomba Mungu hadi tutakapoletewa msimamizi mwingine.
Katika mahubiri yake kwenye ibada hiyo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Mhashamu Jacob Chimeledya aliwataka waumini wote wamtazame Mungu na wamtegemee Mungu kwa sababu wanampenda lakini yeye ameona ni vema ampunzishe mtumishi wake.
“Sote tunajua kuwa katika kipindi chake, Dayosisi hii ilitulia kabisa je tutaruhusu kuondoka anikwake kuzue tena chokochoko? Msiba huu usifike mahali ukaanza kututenganisha na kutoa mwanya wa kuanza kunyoosheana vidole. Tumuombe Mungu atusaidie afute machozi yetu,” alisema.
Askofu John Andrea Simalenga alizaliwa Novemba 30, 1953 na kufariki Novemba 24, 2013 baada ya kuugua kwa siku mbili. Novemba 22, 2013 alijisikia vibaya na alipopimwa aliikutwa na malaria, kisukari na shinikizo la damu. Alilazwa hospitali ya Kibena, Njombe na kuruhusiwa siku iliyofuata lakini Novemba 24 alizidiwa tena na kuaga dunia. Ameacha mjane na watoto wanne.

No comments:

Post a Comment