Mama
mkubwa wa Gervas aliyejitambulisha kwa jina la Martha Lugenge alisema
kuwa vijana hawa walikutana Madibila kila mmoja akiwa katika shughuli
zake ndipo walipoamua kuishi pamoja.
MWANAMKE mkazi wa
kijiji cha Mahango kata ya Madibila wilayani Mbarali mkoani Mbeya aliyefahamika
kwa jina la Jitihada Mamga(20) ameuawa kwa kuchomwa kisu na mumewe
aliyefahamika kwa jina Gervas Kadaga(25) ambaye pia ni mkazi wa kijijini hapo.
Tukio hilo limetokea Novemba 21 majira ya saa 1:00 jioni
baada ya kutokea ugomvi baina ya wapenzi hao ambapo marehemu alikutwa na
majeraha tisa ya kisu katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
Kamanda wa Polisi mkoa wa
Mbeya Bw. Diwani Athumani alisema kuwa marehemu alifia nyumbani kwake ambapo
mtuhumiwa ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya naye amejeruhiwa kwa
kuchomwa na kisu tumboni.
Hata hivyo Kamanda
Athumani alisema kuwa hadi sasa hakijafahamika chanzo halisi cha ugomvi huo
ambapo Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo huku
mtuhumiwa akiwa amewekwa chini ya ulinzi wa polisi katika hospitali ya rufaa ya
Mbeya alikolazwa.
Akizungumza katika
hospitali ya rufaa alikolazwa mama mkubwa wa Gervas aliyejitambulisha kwa jina
la Martha Lugenge alisema kuwa vijana hawa walikutana Madibila kila mmoja akiwa
katika shughuli zake ndipo walipoamua kuishi pamoja.
Alisema yeye alipewa
taarifa za tukio hilo siku inayofuata na kwamba alipofika alikuta ndugu wa
marehemu wameuchukua mwili wa mtoto wao kwa ajili ya taratibu za mazishi na
kwamba hajui chanzo cha ugomvi uliosababisha wapigane visu.
Mama huyo alisema kuwa vijana hao hawajawahi kupata
mtoto na kwamba hawajaanza kuishi pamoja muda mrefu; ''Wote ni
watoto, kwani wameanza kuishi muda mrefu? wamekutana kila mmoja akiwa katika
kazi zake, ndipo walipoanza kuishi kama mke na mume,''alisema
|
No comments:
Post a Comment