KESI ya Mtangazaji Bongo, Maimartha Jesse na Mkurugenzi wa Bendi The African International ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka bado kazi nzito ambapo mshtakiwa (Maimartha) ametakiwa kupeleka ushahidi mahakamani.
Akizungumza kwa masikitiko, Maimartha alisema anaendelea kusubiri siku hiyo ya kupeleka ushahidi ifike kwani anaamini hana makosa kwa sababu hajawahi kumdhalilisha kokote kama alivyoshtakiwa.
“Asha Baraka anataka nimlipe milioni tano sasa sijui hizo fedha zote zimetokana na nini na itakuwaje maana kama ni kudaiana na mimi nitamdai kimwana wangu anayecheza shoo kwake,” alisema Maimartha.
Maimartha Jesse.
Kesi
hiyo ya madai inaendeshwa katika Mahakama ya Mwanzo, Kinondoni, Asha
Baraka amemshtaki Maimartha kwa kile kilichodaiwa kuwa alimdhalilisha
kwenye vyombo vya habari, kesi hiyo itatajwa tena Desemba 19, mwaka huu.-GPL
No comments:
Post a Comment