WATU wanne wamekufa katika matukio manne tofauti jijini Dar es Salaam,
likiwemo la kukutwa maiti ya mtoto mchanga wa kike anayekadiriwa kuwa na
umri wa siku moja.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke Engelbert Kiondo, maiti
ya mtoto huyo iliokotwa juzi saa 6:00 mchana katika maeneo ya Mtoni
Relini Dampo, ambapo ilikutwa imewekwa ndani ya mfuko wa plastiki na
kutupwa katika eneo hilo na mtu asiyefahamika.
Maiti imehifadhiwa katika hospitali ya Temeke na upelelezi unaendelea.
Kamamda Kiondo alisema katika tukio jingine, watu wawili wamekufa katika
maeneo ya Mbande na Chamazi huku chanzo cha vifo vyao kikiwa
hakijajulikana.
Mtu mwingine Juma Kasongo ambaye ni mchungaji wa ng'ombe wanaomilikiwa
na Donald Michael (39) ambaye alikutwa akiwa kitandani kwake akiwa
ameshakufa huku akitokwa na povu mdomoni.
Maiti zimehifadhiwa katika hospitali ya Temeke kwa uchunguzi zaidi na
upelelezi unaendelea. Katika tukio jingine, Dia Haruna (6) amekufa baada
ya kugongwa na gari akivuka barabara katika eneo la Majohe, Wilaya ya
Ilala.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema gari aina
ya Toyota Avensis yenye namba T 636 BYL ikiendeshwa na Njile Mlacha (39)
mkazi wa Majohe, akitoka kwa Diwani kwenda Kwa Mpogo alimgonga mtoto
huyo na kumsababishia majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake.
Majeruhi alikufa muda mfupi baada ya kufikishwa katika hospitali ya
Amana, maiti imehifadhiwa hospitalini hapo na dereva wa gari hili
No comments:
Post a Comment