skip to main |
skip to sidebar
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA: MIAKA KUMI YA MAPINDUZI YA MAWASILIANO TANZANIA
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inasheherekea maadhimisho ya
miaka 10 tangu kuanzishwa kwake huku yakiwemo mafanikio makubwa dhahiri
na ya kujivunia katika sekta ya mawasiliano nchini.
TCRA ilianzishwa
rasmi mnamo tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2013 ili kusimamia Sekta ya
Posta na Mawasiliano ya Elektroniki ikkiwemo simu, utangazaji, wavuti
pamoja na huduma za Posta. TCRA ilkianzishwa kwa Sheria Na. 12 ya mwaka
2003 iliyoziunganisha Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya
Utangazaji Tanzania (TBC).
Mkakati mahususi wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania ni “Kuboresha Maisha ya Watanzania kupitia mfumo
makini na thabiti ili kuhakikisha kunakuwa na huduma za mawasiliano kwa
wote nchini”. Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, Tanzania
imeshuhudia kukua kwa kasi kwa Sekta ya Mawasiliano. Mamlaka ilianzisha
mfumo wa leseni za Muingiliano mnamo tarehe 23 Februari 20005.
Mfumo huu wa leseni za muingiliano (Convergence Lisensing Framework)
umekuwa chachu ya kuongezeka kwa miundombinu mbalimbali ya mawasiliano,
huduma mbalimbali kwa kutumia mtandao wa mawasiliano ikiwemo wavuti
(internet) na utangazaji.
Makampuni ya simu yameongezeka kutoka
kampuni moja ya simu TCRA ilivyoanzishwa mwaka 2003 hadi kufikia
makampuni saba (7) yenye wateja wenye laini za simu takribani milioni 28
kulinganisha na idadi iliyokuwepo miaka kumi iliyopita. Huduma za simu
za mkononi zimebadilisha maisha ya Watanzania kutokana na huduma
mbalimbali zinazopatikana kupitia simu za mkononi. Kuanzia huduma za
kutuma fedha kupitia simu, malipo ya Ankara mbalimbali na huduma
nyingine nyingi zilizobadilisha maisha na uchumi wa wananchi wa taifa
hili.
Sekta ndogo ya Posta nayo haijabaki nyuma kwani kumekuwepo na
ongezeko la watoa huduma kutoka mmoja hadi zaidi ya hamsini wenye kutoa
hduma ndani nan je ya Tanzania. Tunatarajia mabadilikjo makubwa kwa
watanzania hasa baada yan kukamilika kwa mradi wa anwani mpya za makazi
na misimbo ya Posta.
Hali kadhalika, yako mabadiliko makubwa sana
katika msekta ndogo ya utangazaji. Kutoka nchi yetu kuwa na Radio moja
hadi Zaidi ya redio 85. Aidha kutokuwepo kwa Kituo cha Utangazaji wa
Runinga hadi vituo vya utangazaji vipatavyo 26. Watumiaji wa wavuti
(intanet wameongezeka kutoka watumiaji million moja hadi takribani
milioni 8 na ushee. Sekta ya Mawasiliano imekuwa chimbuko la maendeleo
ya nchi kwa kutoa ajira kwa watanzania wengi na hali kadhalika kuongeza
mapata ya serekali kwa tozo na kodi mbalimbali zinazotolewa katika
sekta..
Mamlaka ya Mawasiliano imeshinda tuzo mbalimbali katika
masuala ya Udhibiti na Usimamizi Bora wa Huduma za mawasiliano nchini
katika kipindi cha kuweko kwake miaka kumi iliyopita. Nchi mbalimbali
zimekuja Tanzania kujifunza udhibiti na usumamizi wa masuala nyeti ya
mawasiliano kama vile masuala ya uhamaji kuelekea mfumo mpya wa
utangazaji wa dijitali, Mifumo ya uanzishwaji wa anwani za makazi na
misimbo ya posta, Usimamizi mzuri wa masafa na namba za mawasiliano na
mambo mengine mengi.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA MAADHIMISHO TANGU 25 – 29 NOVEMBER 2013
Katika kusheherekea miaka kumi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,
kutakuwa na maadhimisho ya wiki nzima yenye matukio mbalimbali.
Tukianzia na mkutano huu na waandishi wa habari uliokusudia kutoa
taarifa kwenu na kwa wananchi kuhusu maadhimisho haya, kutakuwa na
matukio kadha wa kadha kuelekea kilele cha sherehe za maadhimisho
yanayotarajiwa kufanyika tarehe 29 Novemba 2013.Maadhimisho haya
yanafanika chini ya kauli mbiu ya; Miaka 10 ya TCRA: Miaka Kumi ya
Mapinduzi Katika Sekta ya Mawasiliano
Kesho tarehe 26 Novemba 2013
kutakuwa na tukio maalumu kwa wafanyakazi wa mamlaka ambapo wale
waliokuwepo tangu wakati wa kuanzishwa kwa TCRA watatunukiwa vyeti
pamoja na zawadi mbalimbali kutambua mchango wao kwa taasisi.
Aidha
siku ya tarehe 27 Novemba 2013; kutakua na sherehe ya kutoa udhamini kwa
wanafunzi wanaosoma vyuo vya elimu ya juu wanaochukua masomo ya
mawasiliano, sayansi na teknolojia. TCRA kwa kipindi cha miaka miwili
mfululizo imekuwa ikitoa udhaminim katika masomo hayo kwa wanafunzi
mahiri kwa nia ya kukuza weledi na kuboresha utumishi katika sekta ya
mawasiliano chini ya kinachoitwa “TCRA ICT SCHOLARSHIPS” kwa wanafunzi
wa digrii ya kwanza, digrii za Uzamili na Uzamivu.
Kuanzia tarehe
27 – 29 Novemba, kutakuwa na maonesho maalumu katika viwanja vya ukumbi
wa mikutano wa Mlimani City ambapo watoa huduma mbalimbali za
mawasiliano nchini wataonesha mafanikio yao na huduma wanazotoa kwa
wananchi. Napenda kuchukua fursa hii kuwasihi waandishi wa habari
kuhudhuria maonesho haya ili kujifunza na kutumia fursa hiyo kuelimisha
jamii ya watanzania kuhusu huduma mbalimbali za mawasiliano
zinazopatikana nchini ili wachangamkie fursa.
Hali kadhalika, katika
maadhimisho haya, TCRA imeandaa washa maalumu ya siku mbili wa wadau wa
mawasiliano kujadili fursa, changamoto pamoja na namna gani kwa pamoja
tunavyoweza kufanya mawasiliano kuwa bora Zaidi nchini mwetu. Warsha
hiyo itafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City na
itafunguliwa rasmi tarehe 28 mwezi huu na Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na utaendelea hadi tarehe 29 Novemba 2013. The
Opening Ceremony will be graced by Dk. Mohammed Gharib Billal.
Wadau mbalimbali wa Mawasiliano kama vile kituo cha Habari cha Tanzania
Network Information Centre (tzNIC), Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote -
Universal Communications Services Access Fund (UCSAF), Wamiliki wa
Vyombo Vya Habari - Media Owners Association of Tanzania (MoAT-
Broadcasting), na Umoja wa Makampuni ya Simu - Mobile Operators
Association of Tanzania (MoAT-Mobile Telephony Companies), Africa Media
Group, Agape Associates and TTCL watawasilisha mada mbalimbali.
Vyombo vya Habari vinakaribishwa katika shughuli zote za maadhimisho ya
Miaka 10 ya TCRA ili kutoa elimu kwa umma lakini pia kama fursa ya
kujionea mafanikio ya sekta ya mawasiliano katika kipindi cha miaka kumi
iliyopita ili kuwawezesha wananchi kufahamu tulikotoka, tunakoenda na
fursa zilizoko katika sekta ili kuboresha maisha yao.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
25th November 2012
No comments:
Post a Comment