Inawezekana Bonta ameamua kujibu ‘diss’ za rapper wa Tamaduni Music Nikki Mbishi aliyekuwa akisema mara kwa mara kuwa Bonta sio Conscious MC?
Katika wimbo huu aliopikwa na Mona Gangster ambao amempa shavu mweusi G Nako aka Warawara, Bonta anasikika akirap katika verse ya kwanza:
“Anajifanya mwana hip maisha yake hayana hop, ni bora kufa na mawazo yanayoishi kuliko kuishi na mawazo yaliyokufa.
Wakisema we ni mkali jua ni mgogo wa chupa, bichwa lisilo na akili ni adhabu kwa miguu.
Unaposema mi sio conscious mtaani watu Buuu, ongea tu..ongea tu dogo mafumbo uoga.
Sikio halipimi neno kama ulimi uonjavyo mboga. Kama kiporo hakiitaji moto mwingi,basi sihitaji nguvu kupambana na hao Wabishi.
Ukinisikiliza utanielewa, ukinielewa utanichukia kwa sababu nakuingia.”
Kama unakumbuka katika moja ya ngoma ya Nikki Mbishi aliwahi kurap, ‘Ukitaja Conscious please usimtaje Bonta’.
Je, ilikuwa ni mistari tu ama ni diss kwa Nikki Mbishi?
Usikilize hapa
No comments:
Post a Comment