KIPA mpya wa Yanga, Juma Kaseja, ameonyesha nidhamu ya hali ya juu kwa kufika katika siku ya kwanza ya mazoezi ya timu hiyo, lakini akapigwa ‘stop’ kuanza kazi katika timu hiyo.
Nassoro Matuzya, ambaye ni Daktari Mkuu wa Yanga, ameliambia Championi Jumatano kuwa Kaseja hataweza kuanza kazi rasmi wiki hii kutokana na tatizo la maumivu ya kifundo cha mguu wake wa kulia.
Matuzya amesema kipa huyo aliyesajiliwa katika kipindi hiki cha dirisha dogo tayari ameshaanza matibabu ya tatizo hilo wiki moja iliyopita ambapo sasa yuko katika wiki ya pili ya tiba hiyo na kuongeza kuwa sasa ataanza rasmi kazi yake hiyo mapema wiki ijayo.
“Tumefurahi kuona amefika katika siku ya kwanza ile jana (juzi), lakini hataweza kuanza kazi, tumemzuia kutokana na haya maumivu yake ya kifundo cha mguu ingawa ameshaanza tiba wiki moja iliyopita,” alisema Matuzya huku akiongeza kwa kusema:
“Wiki hii yupo katika wiki ya pili ya tiba hiyo ambayo inatakiwa aifanye kwa wiki mbili, nafikiri kwa hali nilivyoiona ataweza kuanza kazi rasmi wiki ijayo, kama kila kitu kitakuwa sawa kama hali inavyokwenda sasa.”NA GPL
No comments:
Post a Comment