Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Mdenmark, Kim Poulsen.
Martha Mboma na Amisa Mmbaga KOCHA
Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Mdenmark, Kim Poulsen, ameahidi kuibuka na
ushindi kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Zambia katika michuano ya
Chalenji, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Machakos, Kenya.Akizungumza na Championi Jumatano, Kim alisema wanahitaji kuanza vizuri kwenye michezo ya awali, ukiwemo dhidi ya Zambia kwa kuwa anawaamini vijana wake ambao wengi wana umri mdogo.
Alisema hii ni nafasi yao pekee ya kuonyesha uwezo kwenye michuano hiyo mikubwa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na zaidi wanaomba sapoti kutoka kwa Watanzania waliopo nchini Kenya.
Aliongeza kuwa, kikosi hicho ndicho atakachokitumia kwenye michuano ya kuwania nafasi ya kushiriki Kombe la Mataifa Afrika (Afcon).
“Tunahitaji ushindi kwenye mechi ya awali dhidi ya Zambia na mechi nyingine za makundi ili tufikie robo fainali na kusonga mbele zaidi.
“Hii ni fursa pekee kwa vijana wangu kujiuza kimataifa zaidi kutokana na kiwango watakachokionyesha kwenye michuano hii,” alisema Kim.
Mbali na mchezo huo, Kilimanjaro Stars pia imepangwa na Somalia na Burundi kwenye kundi B.CHANZO GPL
No comments:
Post a Comment