Pages

Saturday, November 9, 2013

Maadhimisho ya Saba ya Mlipa Kodi Zanzibar.



WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais, tawala za Mikoa na Idara maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Haji Omar Kheir akihutubia katika kilele cha wiki ya walipa kodi iliyofanyika katika Hoteli ya Bwawani mjiniZanzibar, kushoto Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ofisi ya Zanzibar, Mcha Hassan na Mwakilishi wa Jumuia ya Wafanyabiashara, wenye viwanda na wakulima, Mbarouk Omar.
 Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ofisi ya Zanzibar, Mcha Hassan akitowa maelezo ya maadhimisho ya Saba ya Mlipa Kodi Tanzania wakati wa kutowa Vyeti kwa Walipakodi Bora kwa mwaka 2013, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Bwawani Zanzibar. 


WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais, tawala za Mikoa na Idara maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Haji Omar Kheir (kushoto) akimkabidhi cheti cha mshindi wa kwanza katika mchango mkubwa wa ulipaji wa kodi Zanzibar, Mwakilishi kutoka kampuni ya Zanzibar Communication (ZANTEL), Aziz Said Ali. Cheti hicho kilitolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ofisi ya Zanzibar katika kilele cha wiki ya walipa kodi iliyofanyika katika Hoteli ya Bwawani
MWAKILISHI wa Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar (SMS) wachapishaji wa Magazeti ya ‘Zanzibar leo’, ‘Zanzibar leo jumapili’ na Zaspoti, Haroub Hussein Khamis (kulia) akipokea cheti maalum kutoka kwa Waziri wa Nchi ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Idara maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Haji Omar Kheir baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ofisi ya Zanzibar kulizawadia Shirika hilo kwa utoaji wa habari za ulipaji wa kodi. Cheti hicho kilitolewa katika kilele cha wiki ya walipa kodi iliyofanyika katika Hoteli ya Bwawani







No comments:

Post a Comment