- AFANYA KIKAO NA WANANCHI
- AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akifafanua jambo wakati wa kikao
maalum cha ndani na wakazi wa eneo la Nyamongo, ambapo wananchi wa eneo
hilo walikuwa wakieleza kero zao na wamiliki wa mgodi wa North Mara .
Ndugu
Elizabeth Malembela akielezea jinsi utaratibu ulivyombovu wa
kuwahamisha na kuwalipa fidia wakazi wanaoishi kando kando ya mgodi wa
North Mara.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisikiliza kwa makini malalamiko
ya wananchi wa Nyamongo juu ya ukiukwaji wa utaratibu na mikataba baina
ya wawekezaji na Wanavijiji.
Mkuu
wa Wilaya ya Tarime Ndugu John Henjewele akiwaelezea wakazi wa Nyamongo
kazi za kikosi kazi (Task force) katika kurahisisha shughuli za
kutathimini ardhi na kuchukua malalamiko ya wananchi dhidi ya wawekezaji
wa mgodi wa North Mara.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia moja ya eneo
linaloaminika kutiririsha maji yenye kemikali kutoka kwenye Mgodi wa
North Mara kwenda kwenye mto Mara na kuhatarisha afya za wananchi.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia kwa karibu kabisa maji
ya kemikali kutoka machimbo ya mgodi wa North Mara kuelekea mtoni.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma jiwe la msingi la ofisi ya
Kikundi cha Bodaboda Nyamongo mara baada ya kuzindua ofisi hiyo.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Ndugu Amos Sagara Nyabikwi
akihutubia wakazi wa Nyamongo wakati wa mkutano wa hadhara ambao Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye aliwaelezea wananchi wa eneo hilo
hatua za awali za kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao zilivyoanza.
Mkurugenzi
wa Kushughulikia Malalamiko dhidi ya Jeshi la Polisi, Magereza,
Uhamiaji,Zimamoto na Uokoaji Ndugu Agustine D. Shio akihutubia wananchi
wa Nyamongo na kuwaambia amesikia malalamiko yao dhidi ya Jeshi la
Polisi na atalifanyia kazi mapema iwezekanavyo na haki zitapatina.
Sehemu ya Wakazi wa Nyamongo wakisikiliza kwa makini hotuba ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi nape Nnauye.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nauye akihutubia wakazi wa Nyamongo
wilayani Tarime na kuwaelezea jinsi alivyoanza rasmi kazi ya kutafuta
ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili wananchi wa Nyamongo.
No comments:
Post a Comment