Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa mji wa Vwawa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika mji huo ambao ndiyo makao makuu ya wilaya ya Mbozi, mkutano huo umehudhuriwa na wananchi mbalimbali wa mji wa vwawa, Katika ziara hiyo Kinana ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiani wa Kimataifa, Akizungumza katika mkutano huo Nape Nnauye amesema Injinia Christopher Chiza Waziri wa Chakula na Ushirika aache kuzungumza na vyombo vya habari badala yake aandae majibu kwa ajili ya kuhojiwa kwenye kikao cha Kamati Kuu kwa sababu kuitwa kwake kwenye kamati kuu ya CCM hakukwepeki, Kutokana na matatizo na malalamiko ya wakulima kuhusu pembejeo, kukopwa mazao yao na suala zima la wakulima kuikataa mbolea ya Minjingu huku wakilazimishwa kuitumia.Kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Dr. Asha Rozi Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki Mh. Godfrey Zambi na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi wakipanda miti katika eneo ambalo zahanati ya kijiji cha Mtunduru kata ya Isansa inajengwa kwa ajili ya kutunza mazingira na kuzuia upepo.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MBOZI -MBEYANape Nnauye akiwahutubia wananchi wa wilaya ya VwawaKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amekaa na wanachama wa CCM kijiji cha Ntunduru Kata ya IsansaDr. Asha Rose Migiro akiwahutubia wanambozi leoWapiganaji Ahmed Michuzi , Richard Mwaikenda na Bashir Nkoromo wakiwa wamepumzika kidogoMkuu wa mkoa wa mkoa wa Mbeya Mh. Abass Kandoro akitoka nyumbani kwa balozi katika kijiji cha NtunduruKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka nyumbani kwa balozi katika kijiji cha NtunduruDr. Asha Rose Migiro akitoka nyumbani kwa balozi katika kijiji cha NtunduruKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa nyumba ya daktari katika kijiji cha Ntunduru kata ya Isansa.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia ngoma za asili ya wanyihaKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimuangalia kijana Huruma Wiliam wa Kata ya Isansa wakati alipokuwa akipita kwenye kamba.Umati wa wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo.
MAWAKALA, VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA HAWARUHUSIWI KUINGILIA MCHAKATO WA
UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA VITUONI
-
*Na Oscar Assenga, TangaMwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji
Jacobs Mwambegele amesema kwamba mawakala, viongozi wa vyama vya sias...
32 minutes ago
No comments:
Post a Comment