Mamia ya
waandamanaji nchini Thailand waliingia kwa nguvu katika makao makuu ya
jeshi mjini Bangkok, ikiwa ni siku ya sita tangu kuanza kwa maandamano
dhidi ya serikali.
Msemaji
wa jeshi amesema waandamanaji walivunja kufuli la mlango mkuu na kuingia
katika eneo la makao makuu hayo ya jeshi. Baadaye waliondoka.
Lakini
kiongozi wa waandamanaji Suthep Thaugsuban amekataa ombi hilo.Alhamisi,
Waziri Mkuu Yingluck Shinawatra aliwataka waandamanaji kuacha maandamano
mitaani, ikiwa ni baada ya waziri mkuu huyo kushinda kura ya kutokuwa
na imani naye iliyopigwa bungeni.
"Hatutaacha waendelee na kazi," mbunge mwandamizi wa zamani wa upinzani alisema hayo katika hotuba yake, Alhamisi.
Waandamanaji wapatao 1,000 waliingia kwa nguvu katika viwanja vya makao makuu ya jeshi mjini Bangkok.
Msemaji wa jeshi Kanali Sansern Kaewkamnerd amesema waandamanaji hawakuingia katika majengo.
Mwandishi
wa BBC, Jonah Fisher, ambaye yupo katika eneo la tukio, amesema
waandamanaji walikusanyika nje ya jengo wakisikiliza hotuba za viongozi
wao waliokuwa katika jukwaa walilojenga.
Walikuwa
wakiomba jeshi liwaunge mkono waandamanaji. "Tunataka kujua jeshi liko
upande gani," Shirika la Habari la Uingereza, Reuters lilimkariri mmoja
wa waandamanaji akisema hivyo.
Serikali imewataka waandamanaji kufanya mazungumzo-lakini ombi hilo limekataliwa.
Mwandishi wetu ameelezea hali hiyo kuwa nzuri na kusema serikali inaonekana kuepuka malumbano.
No comments:
Post a Comment