Harakati za
maandalizi ya ujenzi wa jengo jipya (Terminal 3) la uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), zimekuwa zikiendelea polepole hali
inayowatia shaka wadau wengi wa sekta hii ya usafiri wa anga. Kuanza kwa
ujenzi wa jengo hilo ni jambo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa
sekta ya usafiri wa anga kwani kukamilika kwa jengo hilo kunategemewa
kuleta mabadiliko makubwa sana katika huduma zitolewazo na kuleta
ufanisi mkubwa katika huduma za usafiri wa anga na hatimae kukuza uchumi
wa nchi.
Hivi karibuni
wataalamu na mafundi wa kampuni iliyopewa zabuni ya kujenga jengo hilo,
kampuni ya BAM ya Uholanzi, walionekana wakifanya maandalizi ya mwanzo
ya ujenzi huo ikiwa ni pamoja na kuzungushia uzio baadhi ya maeneo,
upimaji wa ardhi na kubandika michoro yenye kuonesha jinsi taswira ya
jengo hilo itakavyokuwa.
Mtandao wa Aviationtz umeshare picha zifuatazo zikionyesha maeneo mbalimbali ya jengo hilo pamoja njia za ndege.
|
Huu ni muonekano kwa upande wa nje ya jengo na nje ya uwanja. |
|
Hapa ni mahali ambapo abiria watakuwa wakisubiri kabla ya kwenda kupanda ndege (Departure Lounge) |
|
|
Muonekano wa ndani ya jengo |
|
Jinsi patakavyoonekana kutokea angani |
|
Muonekano wa jengo,njia za ndege na maegesho ya magari. |
|
Upande wa maegesho ya ndege |
Ujenzi wa jengo
hilo umepangwa kufanyika kwa awamu mbili. Kukamilika kwa awamu ya kwanza
kutawezesha uwanja huo kufikia uwezo wa abiria mil 3.5 kwa mwaka
tofauti na jengo la sasa ambalo uwezo wake ni abiria mil 1.5 kwa mwaka.
Awamu ya pili itaongeza uwezo huo hadi kufikia abiria mil 6 kwa mwaka.
Baada ya kukamilika jengo hilo, jengo lililopo sasa (Terminal II)
litatumika kwa shughuli za abiria wanaosafiri ndani ya Tanzania tu.
No comments:
Post a Comment