Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, November 25, 2013

TAMKO LA TIMU YA COASTAL UNION KUHUSIANA NA SAKATA LA MCHEZAJI ABDI BANDA



Nimepokea simu nyingi za wapenzi wa Coastal Union pamoja na wanahabari kutaka kujua kuhusu kijana wetu Abdi Banda kuihama timu yetu.
Tayari nimeanza kuudhika, kila siku zinazuka habari mpya kuhusu Banda. Nimezunguza naye amenijibu hajawahi kuzungumza na timu yoyote kuhusu usajili.

Ni kweli Banda ni mchezaji mzuri, lakini tuna mkataba naye wa miaka mitatu, utakapoisha atajua kama anataka kuongeza ama kuhama, lakini si sasa bado tunamuhitaji kuifikisha timu mbali.

Ila kama kuna timu inamuhitaji kwa sasa utaratibu unajulikana, waonane na viongozi wazungumze na si kumfuata mchezaji kwa mlango wa nyuma ni kumuharibia kwa wapenzi wake.

Nimeanza kuudhika, leo nitazungumza na viongozi wa timu pamoja na mwanasheria wetu kuhusu utaratibu. Halafu nitatoa msimamo wa timu. Ikiwa kuna mwanahabari anahusika kuihujumu timu ama klabu ya Yanga ni kweli imefanya mazungumzo na kijana wetu bila kufuata njia sahihi, basi sheria ndiyo itakayozungumza si Coastal Union.

nimeambatanisha picha mbili zikimuonyesha Banda akisaini mkataba wa miaka mitatu na Wagosi wa Kaya Julai 18 mwaka huu.
HAFIDH KIDO
MSEMAJI COASTAL UNION
25 NOV, 2013



No comments:

Post a Comment