KIPA mpya wa Yanga, Juma Kaseja leo asubuhi ametinga katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Bora, Kijitonyama huku kipa mwingine wa timu hiyo akishindwa kufika mazoezini hapo.
Kaseja amesajiliwa na Yanga kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Simba kabla ya kuanza kwa msimu huu na klabu hiyo kukataa kumuongeze mkataba mwingine.
Kipa huyo alifika mazoezini hapo lakini akashindwa kufanya mazoezi kwa kuwa ni majeruhi wa 'enka' hivyo alisalimiana na Kocha Ernie Brandts na maafisa wengine wa klabu hiyo kisha akatimua zake.
Mazoezi binafsi yamharibia kuanza Yanga
Kaseja aliuambia mtandao huu kwamba, kwa sasa yeye ni majeruhi wa enka hivyo hataweza kuichezea Yanga lakini atafanya hivyo baada ya siku mbili kutoka sasa.
"Wakati timu haijaanza mazoezi nilikuwa nafanya mazoezi binafsi hivyo sasa huko ndipo nilipoumia enka na kama unavyoona mguu wangu umevimba hapa naenda kumuona daktari ili anipe huduma zaidi," alisema Kaseja.
Daktari wa Yanga, Nassor Matuzya aliuambia mtandao huu kwamba, Kaseja alimpa taarifa za ugonjwa wake na anadhani anaweza kurejea uwanjani kabla ya wikiendi hii.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, kipa mwingine wa Yanga, Ali Mustapha 'Barthez' hakutokea katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika jana.
Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh alisema hana taarifa za kutokuwepo kwa Barthez mazoezini hapo japokuwa kila mchezaji anafahamu taarifa za kuanza kwa mazoezi hayo.
"Hapa kila mchezaji aliambiwa kwamba leo tunaanza mazoezi sasa hao wengine ambao hawapo hapa sijuhi wana matatizo gani, kwani sina taarifa zao zaidi ya Yule kipa chipukizi Yusuf Abdul anayesumbuliwa na bega," alisema Hafidh.
13 tu waanza mazoezi
Katika mazoezi hayo ya Yanga, ni wachezaji 13 tu waliohudhuria huku wengine wakitarajiwa kufanya hivyo kesho.
Wachezaji waliohudhuria mazoezi hayo ni Nizar Khalfan, Said Bahanuzi, Hussein Javu, Nadir Haroub 'Cannavaro', Jerry Tegete, Oscar Joshua, Bakari Masoud, Ibrahim Job, Simon Msuva, Hamis Thabit Rajab Zahir, Abdallah Mguhi, na Reliants Lusajo. Chanzo: shaffihdauda
No comments:
Post a Comment