Afisa
upelelezi wa wilaya Mbeya mtatiro akishukuru wakazi wa mtaa wa iyela
kwa ushirikiano utulivu waliouonyesha wakati wa zoezi la kutafuta
vidhibiti.
Kijana
Daniel Kossam (21) anatuhumiwa wa kumuua bosi wake Bi,Pelesi Chaula
(32)ambaye alikuwa akiishinaye nyumba moja huko mtaa wa Ilembo kata ya
Iyela mkoani mbeya
Daniel
alikuwa akiuza duka la vifaa vya pikipiki la bi, Pelesi lijulikanalo
kwa jina la 'Twiyanze' lililopo kijiji cha Mbalizi nje kidogo ya jiji la
Mbeya.
Chanzo
cha ugonvi inadaiwa kuwa ni kuchelewa kurudi nyumbani kijana huyo ndipo
Pelesi alipochukua jukumu la kumuuliza jambo lililozua ugonvi katiyao
na kusababisha kifo cha bi.Pelesi Chaula.
Kifo cha marehemu Pelesi kimetokana na kupigwa na kitu chenye ncha kali mwilini mwake.
Wakati mauaji hayo yanafanyika mume wa bi Pelesi Chaula alikuwa safarini wilayani Makete mkoani Iringa.
Baada
ya mauaji hayo Kijana Daniel alichukua simu mbili za marehemu na simu
yake pamoja na fedha kiasi cha 114000/= na kuzitumbukiza chooni kisha
alienda kwa jirani kuwajulisha kuwa walikuwa wamevamiwa na majambazi na
kwamba wamemuua bosi wake huyo.
Majirani
walipofika eneo la tukio walishangaa kuona kuwa hakuana sehemu ya
nyumba iliyokuwa imevunjwa, walipo muuliza Daniel alijibu kuwa alisahau
kufunga milango, baaada ya majibu hayo waliingiwa na mashaka na kuamua
kutoa taarifa polisi.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi Mjumbe wa serikali ya mtaa Bi,Neema
Mwasampeta alisema,' Dan alichelewa kurudi na alifokewa sana,nadhani
hicho ndiyo chanzo cha ugonvi wao'. aliongeza kuwa alimjua kijana huyo
kwa muda wa mwaka mmoja.
Na Uswege Luhanga
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment