Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, November 28, 2013

KINANA AWASILI WILAYA YA MOMBA

 1aKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wana CCM waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Nandanga mahali ambapo ni mpaka wa wilaya za Ileje na Momba akiwa tayari kuendelea na ziara yake ya kikazi katika wilaya ya Momba mkoani Mbeya leo akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MOMBA 2aNape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akisalimiana na Eliakim Simpasa aliyekuwa mbunge wa Mbozi Magharibi mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Nandanga wilayani Momba kushoto ni Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC  Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa 3a Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC  Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa akisalimiana na Eliakim Simpasa aliyekuwa mbunge wa Mbozi Magharibi 4aWananchi waliojitokeza kuupokea msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana 5aDr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC  Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa kushoto na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki  Mh Godfrey Zambi wakiwa katika kikao cha halmashauri kuu ya Wilaya Momba. 6aKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza kikao wakati alipokutana na wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya ya Momba mara baada ya kuwasili katika wilaya hiyo. 7Wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya Momba wakiwa katika kikao hicho. 8Wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya Momba wakiwa katika kikao hicho,


No comments:

Post a Comment