Pages

Sunday, November 3, 2013

UJENZI BARABARA MIKOCHENI WASHIKA KASI, MRADI WA BARABARA YA JOURNALISM WAZINDULIWA

FSA_9738Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Barabara ya Journalism, iliyopo Kata ya Mikocheni yenye urefu wa meta 530, jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mipangomiji na Mazingira wa Manispaa, Richard Chengula, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mikocheni Valence Urassa (kulia kwake) na Mwenyekiti wa Serikali Mtaa wa Ali Hassan Mwinyi, Bernard Rwehabura.
FSA_9743Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (aliyekaa) akiweka saini mkataba wa ujenzi wa Barabara ya Journalism yenye urefu wa meta 530, katika Kata ya Mikocheni, Dar es Salaam jana. Wananoshuhudia (kutoka kulia) ni Mhandisi Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Baraka Mkuya, Mwenyekiti wa Kamati ya Mipangomiji na Mazingira Kata ya Mikocheni, Richard Chengula (mwenye kofia) na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mikocheni, Valence Urassa (kushoto)FSA_9753Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (katikati) akimkabidhi zana za kazi Mhandisi Mkuu wa Manispaa hiyo, Baraka Mkuya kwa ajili ya kusimamia ujenzi wa Barabara ya Journalism katika Kata ya Mikocheni yenye urefu wa meta 530 mara baada ya kusaini mkataba wa ujenzi wa Barabara hiyo Dar es Salaam jana. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Kata ya Mikocheni, Valence UrassaFSA_9764Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (wa pili kulia) akipewa maelezo na Mhandisi Mkuu wa Manispaa hiyo, Baraka Mkuya kuhusu ujenzi wa Barabara ya Journalism katika Kata ya Mikocheni yenye urefu wa meta 530 mara baada ya kusaini mkataba wa ujenzi wa Barabara hiyo Dar es Salaam jana. Kulia ni Mhandisi wa Barabara Manispaa hiyo, Koyoya Fuko na Mwenyekiti wa Kamati ya Mipangomiji na Mazingira, Richard Chengula (mwenye kofia).FSA_9724Wasanii wa kikundi cha Masai wakitumbuiza wakati wa sherehe za uzinduzi wa mradi huo wa Barabara ya Journalism.
Ujenzi wa Barabara za ndani kwa kiwango cha lami katika Kata ya Mikocheni Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam unaendelea kushika kasi baada ya Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Yusuf Mwenda jana kusaini mkataba wa ujenzi wa Barabara ya Journalism yenye urefu wa mita 530 baina ya manispaa hiyo na Mkandarasi, kampuni ya MS Skol.
Barabara hiyo ni miongoni mwa nne zenye urefu wa Kilometa 2.68 ambazo zimo kwenye ujenzi wa kiwango hicho kwa gharama ya shilingi bilioni 2.65 fedha za Serikali zilizotolewa kwa Halmashauri hiyo.
Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo, Meya Yusuf Mwenda amewataka Watendaji Kata na Wenyeviti wa Mitaa hiyo kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi ili aweze kukamilisha ujenzi huo ndani ya muda waliokubaliana wa miezi mitatu.
“Watendaji na Wenyeviti hakikisheni mnasimamia ujenzi huu ukamilike ndani ya muda tuliokubaliana ili wakazi wa Kata hii (Mikocheni) waanze kula matunda ya Serikali kwa kuwaboreshea maisha yao.” Alisema na kuongeza,
“Serikali yetu chini ya Rais Jakaya Kikwete inahakikisha kutekeleza Ilani yake ya uchaguzi, nah ii ni mojawapo ya utekelezaji huo hivyo niwaombe wakazi wa Kata hii kuonesha ushirikiano na mkandarasi kwani najua kuna baadhi ya wakazi waliongia kwenye mipaka ya Barabara wataathirika. Ili kuepuka hilo, naomba wale wote ambao wanaona wameingia kwa makusudi kwenye mipaka ya Barabara waanze kuondoka wenyewe.” Alisema.
Jumla ya Barabara nne za Kata hiyo ya Mikocheni zipo kwenye ujenzi huo ambao tayari mkandarasi ameanza ujenzi ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Februari mwakani.
Barabara hizo ni Feza (mita 750), Chukwi (mita 800), Serengeti (mita 600) na Journalism (mita 530) ambazo zinakamilisha jumla ya Kilometa 2.68.

No comments:

Post a Comment