Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akizungumza wakati wa uzinduzi
wa ujenzi wa Barabara ya Journalism, iliyopo Kata ya Mikocheni yenye
urefu wa meta 530, jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mipangomiji na
Mazingira wa Manispaa, Richard Chengula, Ofisa Mtendaji wa Kata ya
Mikocheni Valence Urassa (kulia kwake) na Mwenyekiti wa Serikali Mtaa wa
Ali Hassan Mwinyi, Bernard Rwehabura.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (aliyekaa) akiweka saini mkataba
wa ujenzi wa Barabara ya Journalism yenye urefu wa meta 530, katika
Kata ya Mikocheni, Dar es Salaam jana. Wananoshuhudia (kutoka kulia) ni
Mhandisi Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Baraka Mkuya, Mwenyekiti wa
Kamati ya Mipangomiji na Mazingira Kata ya Mikocheni, Richard Chengula
(mwenye kofia) na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mikocheni, Valence Urassa
(kushoto)Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (katikati) akimkabidhi zana za
kazi Mhandisi Mkuu wa Manispaa hiyo, Baraka Mkuya kwa ajili ya kusimamia
ujenzi wa Barabara ya Journalism katika Kata ya Mikocheni yenye urefu
wa meta 530 mara baada ya kusaini mkataba wa ujenzi wa Barabara hiyo Dar
es Salaam jana. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Kata ya Mikocheni, Valence
UrassaMeya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (wa pili kulia) akipewa maelezo
na Mhandisi Mkuu wa Manispaa hiyo, Baraka Mkuya kuhusu ujenzi wa
Barabara ya Journalism katika Kata ya Mikocheni yenye urefu wa meta 530
mara baada ya kusaini mkataba wa ujenzi wa Barabara hiyo Dar es Salaam
jana. Kulia ni Mhandisi wa Barabara Manispaa hiyo, Koyoya Fuko na
Mwenyekiti wa Kamati ya Mipangomiji na Mazingira, Richard Chengula
(mwenye kofia).Wasanii wa kikundi cha Masai wakitumbuiza wakati wa sherehe za uzinduzi wa mradi huo wa Barabara ya Journalism.
Ujenzi
wa Barabara za ndani kwa kiwango cha lami katika Kata ya Mikocheni
Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam unaendelea kushika kasi baada ya
Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Yusuf Mwenda jana kusaini mkataba wa
ujenzi wa Barabara ya Journalism yenye urefu wa mita 530 baina ya
manispaa hiyo na Mkandarasi, kampuni ya MS Skol.
Barabara
hiyo ni miongoni mwa nne zenye urefu wa Kilometa 2.68 ambazo zimo
kwenye ujenzi wa kiwango hicho kwa gharama ya shilingi bilioni 2.65
fedha za Serikali zilizotolewa kwa Halmashauri hiyo.
Akizungumza
mara baada ya kusaini mkataba huo, Meya Yusuf Mwenda amewataka
Watendaji Kata na Wenyeviti wa Mitaa hiyo kuhakikisha wanamsimamia
mkandarasi ili aweze kukamilisha ujenzi huo ndani ya muda waliokubaliana
wa miezi mitatu.
“Watendaji
na Wenyeviti hakikisheni mnasimamia ujenzi huu ukamilike ndani ya muda
tuliokubaliana ili wakazi wa Kata hii (Mikocheni) waanze kula matunda ya
Serikali kwa kuwaboreshea maisha yao.” Alisema na kuongeza,
“Serikali
yetu chini ya Rais Jakaya Kikwete inahakikisha kutekeleza Ilani yake ya
uchaguzi, nah ii ni mojawapo ya utekelezaji huo hivyo niwaombe wakazi
wa Kata hii kuonesha ushirikiano na mkandarasi kwani najua kuna baadhi
ya wakazi waliongia kwenye mipaka ya Barabara wataathirika. Ili kuepuka
hilo, naomba wale wote ambao wanaona wameingia kwa makusudi kwenye
mipaka ya Barabara waanze kuondoka wenyewe.” Alisema.
Jumla
ya Barabara nne za Kata hiyo ya Mikocheni zipo kwenye ujenzi huo ambao
tayari mkandarasi ameanza ujenzi ambao unatarajiwa kukamilika mwezi
Februari mwakani.
Barabara
hizo ni Feza (mita 750), Chukwi (mita 800), Serengeti (mita 600) na
Journalism (mita 530) ambazo zinakamilisha jumla ya Kilometa 2.68.
No comments:
Post a Comment